Makamu mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amewasili jijini Nairobi nchini Kenya akitokea nchini Ubelgiji anakoishi ikielezwa kuwa yupo nchini humo kwa ajili ya uzinduzi wa kitabu chake cha Vivuli- Bunge na uwajibikaji kwa Afrika Mashariki, utakaofanyika kesho Ijumaa Juni 25,2021 katika hoteli ya Windsor.
Mwanasheria wake, Profesa George Wajackoya amethibitisha uwepo wa Lissu Nairobi Kenya na kwamba uzinduzi wa kitabu hicho utafanyika kesho Ijumaa Juni 25,2021.
Social Plugin