TANGAZO LA MASOMO KIDATO CHA TANO 2021/2022
Shule ya Sekondari Buluba iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga, Mkoa wa Shinyanga inawatangazia nafasi za masomo ya kujiunga Kidato cha Tano kwa mwaka wa taaluma 2021/2022.
Masomo yataanza rasmi tarehe 5 Julai, 2021.
Shule hii iko Mkabala na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na ina mandhari nzuri ya kujifunza katika tahasusi za HKL, HGL, HGK, CBG, PCB na PCM.
Pia ina darasa la jioni kwa Watahiniwa wa Kujitegemea katika Tahasusi za HKL, HGL na HGK.
Ada yetu ni nafuu mno: Kutwa (Day) ni Tshs. 750,000/= tu (hulipwa mara mbili kwa mwaka) na Hosteli (Boarding) ni Tshs. 1,500,000/= (hulipwa mara nne kwa mwaka).
Kwa Watahiniwa wa Kujitegemea: Ada ni Tshs. 400,000 tu kwa mwaka na hulipwa mara mbili.
Ewe mzazi, mlete mwanao apate elimu bora kutoka Shule hii kongwe katika Mkoa na Ukanda huu wa Ziwa Viktoria.
Kwa mawasiliano zaidi, tafadhali tupigie kwa Simu zifuatazo:
0754048182 Bw. Alexander Yegela (Mkuu wa Shule)
Au
0788107001 Bw. Ferdinand Chuwa (Makamu Mkuu wa Shule)
NYOTE MNAKARIBISHWA
Social Plugin