DC MBONEKO ATOA MSAADA WA VITI NA MEZA KWA AJILI YA WALIMU SHULE ZA SEKONDARI NGOKOLO NA MWAWAZA….AWATAKA KUONDOA 'F'


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kushoto akikabidhi Meza 12 na Viti viwili kwa ajili ya matumizi ya walimu katika Shule ya Sekondari Ngokolo, kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Malale Masali akiwa na walimu wa shule hiyo.

Na Marco Maduhu, Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ametoa msaada wa Viti na Meza, kwa ajili ya matumizi ya walimu, katika shule ya Sekondari Ngokolo na Mwawaza.

Mboneko ametoa msaada wa Viti na Meza hizo leo, ikiwa ni sehemu ya ahadi yake aliyoitoa wakati alipokuwa akifanya ziara ya kutembelea sekta ya elimu, na kutafutia ufumbuzi changamoto alizokuwa akikumbana nazo.

Alisema ameamua kutoa viti na meza hizo, ili kuwaondolea changamoto walimu kutumia viti na meza za wanafunzi wakati wa kusahihisha mitihani, madaftari na hata kuandaa masomo.

"Katika shule hii ya sekondari Ngokolo nimetoa meza 12 na viti viwili, sekondari ya Mwawaza meza nne na viti nane kama nilivyoahidi, ili mfundishe katika mazingira rafiki na kufaulisha wanafunzi,"alisema Mboneko.

"Niwahakikishieni tu walimu, serikali itaendelea kujali maslahi yenu, hivyo naomba mjitume kufundisha kwa bidii na kuondoa 'F', nataka wanafunzi wote wafaulu," aliongeza.

Nao Wakuu wa Shule Malale Masali wa Sekondari Ngokolo, na Juliana Limbe wa Mwawaza, kwa nyakati tofauti walisema hawana cha kumlipa Mkuu huyo wa Wilaya, ila wanamuahidi matokeo mazuri ya kidato cha nne mwaka huu na hakutakuwa na F.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Daudi Mkumbo, alimpongeza mkuu huyo wa Wilaya, kwa kazi nzuri ambayo anaifanya ya kutatua changamoto za elimu.


Aidha Madiwani wa Kata hizo Mbili, Victor Mkwizu wa Ngokolo, na Juma Nkwabi wa Mwawaza walimpongeza Mboneko, na kuahidi kuendelea kushirikiana naye katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na walimu na baadhi ya wajumbe wa bodi ya shule ya Sekondari Ngokolo, mara baada ya kumaliza kukabidhi viti na meza.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na walimu wa shule ya Sekondari Ngokolo na kuwataka wafundishe kwa bidii, huku Serikali ikiendelea kuwatatulia changamoto zao.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na walimu pamoja na wanafunzi katika shule ya Sekondari Mwawaza.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Malale Masali, akishukuru kupewa Vita na Meza na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwawaza Juliana Limbe, akitoa shukrani kwa kupewa viti na meza na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Diwani wa Ngokolo Victor Mkwizu, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kupewa Viti na Meza.
Diwani wa Mwawaza Juma Nkwabi, akizungumza kwenye hafla hiyo ya Shule ya Sekondari Mwawaza kupewa Viti na Meza.
Kaimu Afisa elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Daudi Mkumbo, akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kwa kusaidia kutatua changamoto sekta ya elimu.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kushoto akikabidhi Meza 12 na Viti viwili kwa ajili ya matumizi ya walimu katika Shule ya Sekondari Ngokolo, kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Malale Masali akiwa na walimu wa shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kushoto, akikabidhi Viti Viwili kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Malale Masali kulia, kwa ajili ya matumizi ya walimu shuleni hapo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kushoto, akikabidhi Meza Nne kwa ajili ya matumizi ya walimu katika shule ya Sekondari Mwawaza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kushoto akikabidhi viti nane kwa ajili ya matumizi ya walimu katika shule ya Sekondari Mwawaza.
Muonekano wa meza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kulia, akimpatia zawadi ya fedha Mwalimu wa shule ya Sekondari Ngokolo Ernest Mponda kutokana na kufundisha vizuri na kupunguza 'F' shuleni hapo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kulia akimkabidhi zawadi ya fedha Mwalimu Alodi Katabalo kutokana na kujituma kufundisha vizuri shuleni hapo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kulia, akimkabidhi zawadi ya fedha Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Malale Masali, kutokana na kusimamia vizuri taaluma shuleni hapo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua ujenzi wa vyumba viwili ya madarasa na ofisi moja ya walimu katika shule ya sekondari Ngokolo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua ujenzi wa maabara ya Sayansi katika Shule ya Sekondari Mwawaza.
Ukaguzi ujenzi wa maabara ya sayansi ukiendelea.
Ukaguzi ujenzi wa maabara ya sayansi ukiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipiga picha ya pamoja na walimu katika shule ya Sekondari Ngokolo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kushoto, akipiga picha ya pamoja na Mwalimu Ernest Mponda ambaye ni miongoni mwa walimu wanaofanya vizuri kufundisha wanafunzi shuleni hapo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipiga picha ya pamoja na walimu na wanafunzi katika shule ya Sekondari Mwawaza.
Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwasili katika shule ya Sekondari Ngokolo, kwa ajili ya kutimiza ahadi yake ya kutoa Viti na Meza kwa ajili ya matumizi ya walimu shuleni hapo.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post