Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HII NDIYO MIJI YA GHARAMA ZAIDI DUNIANI KUISHI MWAKA 2021


Iwapo unafikiria kuhamia katika taifa jingine, orodha hii inaweza kukusaidia kufanya maamuzi ya kifedha.

Mji mkuu wa Turkimenistan , katikati mwa bara Asia , umeorodheshwa kuwa mji ghali zaidi duniani kwa wafanyakazi wa kigeni.

Ashgabat , mji wa watu milioni moja , umeongoza orodha ya 2021 ya miji yenye gharama kubwa ya kuishi kulingana na kampuni ya Mercer.

Orodha hiyo inauweka mji wa Ashgabat juu ya miji iliokuwa na gharama ya juu kuishi mwaka uliopita kama vile Hong Kong, ambao umekuwa wa pili, ukifuatiwa na mji wa Beirut nchini Lebanon na Tokyo nchini Japan.

Ripoti hiyo ya kila mwaka inaorodhesha miji 209 kulingana na gharama ya matumizi kama vile nyumba , uchukuzi na chakula.

Mercer ilitathimini zaidi ya bidhaa 200 na huduma katika ripoti hiyo, ambayo inalenga kusaidia biashara na serikali duniani kubaini jinsi zitakavyowalipa wafanyakazi wa kigeni.
Mwaka uliopita Hongkong iliongoza orodha hiyo

Baadhi ya miji iliyopo katika 10 bora ni vituo vya kiuchumi ambapo ukuaji umesababisha bei ya nyumba kupanda pamoja na gharama nyengine za maisha.

Lakini Ashgbat umetajwa kuwa ghali zaidi kutokana na kukumbwa na matatizo ya kiuchumi badala ya maendeleo.

Kwanini mji huo unaongoza orodha hiyo?

Afisa wa kampuni ya Mercer Jean-Philippe aliambia chombo cha habari cha AFP kwamba mfumuko wa kiwango cha juu unaelezea sababu ya Ashgbat kuwa ghali zaidi duniani.
Zúrich ni kituo cha kifedha

Turkmenistan, ikijulikana kwa uongozi wake wa kiimla na hifadhi zake za gesi , umekumbwa na mzozo wa kiuchumi wa muda mrefu ambao umesababisha raia wengi kuwa masikini.

Awali ikiwa chini ya muungano wa Usovieti , taifa hilo linategemea gesi asilia ili kuuza kwa Urusi.

Mzozo wa kiuchumi unaoikumba kwa sasa umesababishwa , na bei ya chini ya gesi.

Kushuka kwa bei za kawi duniani mwaka 2014 kulisababisha mfumuko na kupanda kwa bei za vyakula.

Mnamo mwezi Septemba mwaka uliopita, ripoti ya shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch HRW ilisema kwamba mlipuko wa virusi vya corona uliongeza tatizo la ukosefu wa chakula nchini Turkmenistan.
Umaarufu wa mji wa Shanghai ni kwamba una majumba mengi marefu

"Tatizo hilo la ukosefu wa chakula ambalo liliendelea tangu mwaka 2016, lilikuwa baya zaidi , huku watu wakilazimika kupiga foleni kwa saa kadhaa ili kununua chakula cha bei ya chini , huku wengine wakilazimika kuondoka bila chochote'', ilisema ripoti.

Licha ya hilo, serikali ya Turkmenistan ilianza upanuzi wa mji wa Ashgbat mnamo mwezi Mei.

Rais wa zamani Gurbanguly Berdymukhamedov aliahidi kuufanya mji huo miongoni mwa miji ilioendelea zaidi duniani.

Je miji mingine iko wapi katika orodha hiyo?

Mji mkuu wa Lebanon , Beirut , ulipanda kutoka katika nafasi ya 45 mwaka uliopita hadi nafasi ya tatu 2021.

Mercer imetaja hatua hiyo kutokana na sababu kadhaa , ikiwemo msukosuko wa kisiasa wa hivi karibuni na tatizo la kiuchumi la muda mrefu.

"Mlipuko wa virusi vya corona na mlipuko wa bandari ya Beirut 2020 uliongeza tatizo hilo la kiuchumi na kusababisha mfumuko mkubwa , ilisema Mercer.

Miji mitatu ya Uswizi ilikuwa katika 10 bora mwaka 2020, ikiwemo Zurich ambayo ilishuka hadi katika nafasi ya 5 katika orodha ya mwaka huu.

Kati ya miji ilio ghali zaidi, mji wa Shanghai ulipanda hadi nafasi ya sita huku mji mkuu Beijing ukipanda hadi nafasi ya tisa.

Singapore, taifa la kisiwani linalojulikana kwa sekta ya kifedha ilioimarika , ilikuwa katika nafasi ya saba.

Chini ya orodha hiyo ni mji mkuu wa Kyrgyz, Bishkek uliowekwa kuwa mji ghali zaidi kwa wafanyakazi wa kigeni.

Chanzo - BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com