Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SBFIC YATOA MAFUNZO YA FEDHA KWA WAJASIRIAMALI NA VIKUNDI VYA SACCOS



Na Lucas Raphael - Tabora

Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Savings Bank Foundatin For International Cooperation  (SBFIC) Tanzania imewasaidia  wanachama  wa vikundi  vya Saccos na wajasiriamali wapatao 3000 kupata elimu ya kuhusiana na masuala ya kifedha ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kujikomboa katika umaskini wa kipato.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkazi SBFIC, Stephen  Safe wakati akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alipotembela  banda  siku ya Maadhimisho ya sherehe ya siku ya Ushirika Duniani kwenye viwanja vya Nane Nane Ipuli Mkoani Tabora.

 

Safe alisema mafunzo hayo yanalenga uhalisia wa biashara katika maisha ya kawaida ya wananchi ambapo mafunzo hayo yanawapa walengwa maarifa na ustawi wa taaluma za biashara zao, kitu kinachopelekea kuwa wateja wa kuaminika zaidi kwa taasisi za kifedha na ushirika wa akiba na mikopo.

 

Alisema kupitia mafunzo hayo , taasisi hiyo hufundisha wafanyakazi wa ushirika  kufanya michezo ya biadhara na hivyo kupelekea udhibiti .

 

Aidha Safe alisema mafunzo hayo ya kuwapa elimu ya masuala ya kifedha ambayo  yalifundishwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari  3, 500 waliopo katika mikoa ya Mwanza na  wilaya ya Karagwe mkoa Kagera.

 

Naye Afisa Mwandamizi wa mafunzo ya elimu ya fedha  Kalunde Kapaliswa alisema shughuli zimetoa  mafanikio kwa kuimarisha Taasisi za mashirika ya washirika wakuu ambao ni Tume ya ushirika ,SCCULT, TCDC ,SELF, ACB na TAMFI  zinazofanywa na SBFIC nchini Tanzania .

 

Alisema hali hiyo imeboresha muundo na shughuli za washirika na kuhakikisha uimara wao nchini Tanzania.

 

Alisema mafanikio ni makubwa ambayo yalisababisha washirika wao ambao ni  SELF MF kutoka kuwa mradi wa maendeleo na kuwa shirika linalolenga biashara na baadaye kuungana  na Taasisi zingine za kifedha .

 

Alifafanua kuwa uingizwaji wa sekta ndogo ndogo za fedha na vyama vya ushirika wa akiba na mikopo katika mfumo wa kidigitali mwaka 2019.

 


Hata hivyo Naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe, aliipongeza Taasisis hiyo kwa kutoa elimu ya kifedha kwa vyama vya akiba na mikopo nchini.

Alisema ni jambo jema kwa taasisi hiyo kutoa elimu ya fedha kwa vitendo jambo ambalo hakuna sehemu nyingine iliwezea kufanya hivyo

Naibu waziri huyo alitoa wito kwa taasisi zingine za kifedha kuiga mfano huo na kuweza kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com