Video ya muhubiri maarufu TB Joshua akitabiri kwamba hataweza kusherehekea siku yake ya kuzaliwa Juni 12,2021 kama kawaida imeibuka kwenye mtandao wa kijamii.
Haya yanajiri baada ya Mhubiri huyo maarufu mwenye umri wa miaka 57, kupumua pumzi yake ya mwisho Jumamosi, Juni 5,2021 lakini bado chanzo cha kifo chake hakijafichuliwa.
Kulingana na video hiyo ambayo ilichapishwa kwenye Twitter Alhamisi, Juni 3,2021 mtumishi huyo wa Mungu alikuwa anatazamiwa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa akitimia umri wa miaka 58 Jumamosi, Juni 12,2021.
Hata hivyo, pasta huyo Mnigeria alisema kutokana na sababu zisizoweza kuepukika ambazo hakuzitaja, alisema hatasherehekea siku hiyo. "Kwa watu wote kote ulimwenguni Juni 12, inakaribia na kama mjuavyo mimi ni mtu wa watu, kwa hivyo shida ya mmoja ni ya kila mtu. Kama ilivyo, unaweza kutambua kuwa haikuwa rahisi kwangu kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa. Watu ambao wanataka kuja wamezuiwa na hali hiyo," alisema Joshua.
Badala yake aliamua kufunga na kuomba kwa ajili ya siku hiyo spesheli. Wakati wa siku hiyo, aliwahimiza wafuasi wake kuwakumbuka wasiojiweza. Taarifa katika ukurasa wake wa Facebook zilisema alifariki Jumamosi baada ya kumtumikia Bwana kwa kipindi kirefu.
"Mnamo Jumamosi, Juni 5, 2021. Nabii TB Joshua alizungumza kwenye mkutano wa Emmanuel TV Partners kuhusu wakati wa kuja hapa kufanya maombi na wakati wa kurudi nyumbani kwa ibada," taarifa hiyo ilisema.
"Mungu amemchukua mtumishi wake Nabii TB Joshua nyumbani kama inavyotakikana. Siku zake za mwisho duniani zilikuwa za huduma kwa Mungu. Hili ndilo alizaliwa kufanya, na alifariki akifanya hivyo," taarifa iliongeza.
TB JOSHUA AT 58: Important Birthday Message!
— TB Joshua (@SCOANTBJoshua) June 3, 2021
"Happy Birthday to you! Viewers all over the world, June 12th is around the corner. As you know, I am a man of the people. So, the wound of one is the wound of all. pic.twitter.com/W0xYAzmUsw
HUYU NDIYE TB JOSHUA..MHUBIRI MWENYE MIUJIZA MINGI ALIYEKAA TUMBONI KWA MAMA YAKE MIEZI 15
Social Plugin