Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Pili Hassani Mnyima akimkabidhi Cheti Afisa Mwandamizi wa Miradi kutoka Benki ya Maendeleo TIB, Sonia Mlaki (kushoto) baada ya Benki hiyo kushika nafasi ya kwanza katika kipengele cha Benki zenye huduma zenye tija za maendeleo ya nchi kwa ujumla wake tofauti na benki zingine zilizoshiriki maonyesho hayo ya biashara ya 8 yaliyofanyika kitaifa mkoani Tanga. TIB Development Bank pia imeshika nafasi ya tatu katika kipengele cha huduma za bima.
Afisa Mwandamizi wa Miradi kutoka Benki ya Maendeleo TIB, Sonia Mlaki akionesha cheti
Afisa Msimamizi wa miradi kutoka Benki ya Maendeleo TIB Sonia Mlaki akiwa na Afisa Mwandamizi Idara ya Masoko na Mahusiano Carlos Nathaniel Ntangeki kwenye Maonyesho ya biashara ya 8 ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Tanga.
Social Plugin