Benki ya TPB imetoa msaada wa vyakula katika shule ya msingi ya Pongwe mkoani Tanga yenye wanafunzi wenye mahitaji maalum ikiwa ni sehemu ya kushiriki nao katika maadhimisho y siku ya Mtoto wa Afrika.
Meneja wa Benki ya TPB tawi la Tanga Patrick Swenya amesema wameamua kuungana na mataifa mengine barani Afrika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa kila ifikapo Juni 16 kwa kutoa msaada wa chakula kwa watoto hao na kwamba kuwa wataendelea kutoa msaada kwa watoto hao na wamekuwa wadau wakubwa katika shule hiyo wanapohitaji msaada.
Social Plugin