Kijana Machage Samson (22) mkazi wa kijiji cha Nyamisingisi wilayani Serengeti mkoani Mara amefungwa miaka 30 na Mahakama ya Wilaya ya Serengeti kwa kumpa mimba mwanafunzi wa darasa la saba.
Hukumu katika kesi ya Jinai namba 280/2020 imesomwa na Hakimu Mkazi wa Wilaya Judith Semkiwa baada ya mshtakiwa kutiwa hatiani kwa kosa la kumpa mimba mwanafunzi wa darasa la saba shule ya Msingi Nyamisingisi mwenye umri wa miaka (16) na kumzuia asiendelee na masomo.
Mwendesha Mashitaka wa Jamhuri Faru Mayengela amesema,kati ya Januari na Julai 2020 mshitakiwa anadaiwa kujihusisha kimapenzi na mwanafunzi huyo,na kuwa alikuwa akitegea mama wa mtoto huyo alipokuwa akienda kuuza karanga stendi ya Issenye anamchukua na kwenda kufanya naye ngono,ameiomba mahakama itoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Samson katika utetezi wake amesema,hizo ni chuki zinazotokana na ugomvi wa mama yake na mama wa mtoto ,hata hivyo maelezo yake hayakuweza kuishawishi mahakama imwonee huruma kwa kuwa hakumtaja kama shahidi wakati wa kesi na alijitetea mwenyewe.
Chanzo :Serengeti Media Centre
Social Plugin