Utando mkubwa wa buibui uliofinika miti umetanda karibu na maeneo ya miji iliokumbwa na mfauriko nchini Australia.
Wakazi katika eneo la Gippsland wanasema kwamba utando huo ulijitokeza baada ya siku kadhaa ya mvua kubwa.
Katika eneo moja , utando huo wa buibui ulifunika takriban kilomita moja ya barabara.
Wataalam wanasema kwamba mbinu inayoitwa 'Balloning' ambapo mabuibui hurusha silk ili kupanda katika maeneo ya juu ndio ilisababisha utando huo.
Dkt Ken Walker, mtunzaji mwandamizi wa wadudu kutoka jumba la Makumbusho la Victoria, alisema kuna uwezekano mamilioni ya buibui walikuwa wamerusha nyuzi zao kwenye miti iliyo karibu.
"Buibui wanaoishi ardhini hutaka kuondoka ardhini kwa haraka sana. Hivyobasi wanaporusha nyuzi hizo huinuka na kushika mimea na wanaweza kutoroka," aliambia gazeti la The Age.
Utando wa buibui wafunika barabara na miti
Diwani mmoja wa eneo hilo, Carolyn Crossley, alisema alikuwa ameenda katika tuta la ziwa moja siku ya Jumatatu jioni kuangalia uharibifu uliofanywa na mafuriko, na alishangazwa na hali hiyo .
Bi Crossley alisema alikuwa ameona tukio kama hilo hapo awali, lakini sio kwa kiwango kikubwa kama hicho.
"Haikuwa inatisha - ilikuwa nzuri. Kila kitu kiligubikwa na utando huo wa buibui, kote kwenye miti na uzio," aliiambia BBC.
Mkazi mwingine wa eneo hilo, Amanda Traeger, aliambia BBC kwamba familia yake ilidhani kwamba kulikuwa na neti kandokando ya barabara.
Alisema utando huo ulionekana kama karatasi moja, au kitambaa ambapo buibui wadogo walitambaa.
"Kwa kuwa haukujitenga - ilikuwa kama buibui hawa walikuwa wameshirikiana kufanya usanikishaji wa mazingira ," alisema
Mkazi mwingine wa eneo hilo, Amanda Traeger, aliambia BBC kwamba familia yake ilidhani kwamba kulikuwa na neti kandokando ya barabara.
''Niliwahi kuona kitu kama hiki awali lakini sio kwa ukubwa huu na kizuri hivi''
Utando huo maridadi unatarajiwa kusambaratika baadaye wiki hii.
Mvua kubwa na upepo mkali ulikumba sehemu kubwa ya eneo la Victoria, na kusababisha mafuriko na uharibifu mkubwa wiki iliyopita.
Watu wawili walipatikana wakiwa wamekufa katika magari yao katika visa tofauti vya mafuriko.
Mamlaka imeelezea kwamba kimbunga hicho kimesababisha janga huku nyumba nyingi katika jimbo hilo zikiwa hazina umeme.
CHANZO - BBC SWAHILI
Social Plugin