Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Venant Mboneko
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Jumamosi Juni 19,2021 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilayanchini ambapo amewabadilisha vituo vya kazi baadhi, ameingiza sura mpya na kuwarudisha waliowahi kushika nafasi hizo.
Katika orodha hiyo, Kwa upande wa mkoa wa Shinyanga, Rais Samia amewateua Joseph Modest Mkude kuwa Mkuu wa wilaya ya Kishapu akichukua nafasi ya Nyabaganga Talaba, Festo Kiswaga kuwa mkuu wa wilaya ya Kahama akichukua nafasi ya Anamringi Macha huku Jasinta Mboneko akibakizwa katika nafasi ya Ukuu wa wilaya ya Shinyanga.
Social Plugin