Mwili wa mwanaume anayedaiwa kuwa ni mfugaji mkazi wa kijiji cha Arirai wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha, Sabore Shumbi (44) umekutwa pembeni ya duka la kuuza vinywaji vikali katika kijiji cha Haydom wilaya ya Mbulu Mkoa wa Manyara ukiwa na majeraha kichwani kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Merrisone Mwakyoma amesema chanzo cha kifo hicho hakijajulikana akisema mwili huo umekutwa na majeraha matatu kichwani na kwamba watu waliokuwa wakipita eneo hilo ndio walioutambua mwili huo na kutoa taarifa polisi.
"Jina la mmiliki wa kibanda hicho linahifadhiwa wakati huu tunaoendelea na uchunguzi kwa sababu tangu kifo chake hakuna muuzaji wala mmiliki wa duka aliyeonekana wala kufungua duka",amesema Kamanda Mwakyoma
Social Plugin