Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Jumamosi Juni 19,2021 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilayanchini ambapo amewabadilisha vituo vya kazi baadhi, ameingiza sura mpya na kuwarudisha waliowahi kushika nafasi hizo.
Katika uteuzi huo Rais Samia pia amewateua baadhi ya waliokuwa wabunge lakini kwa sababu mbalimbali wakashindwa kurejea bungeni. Wateule hao ni Joshua Nassari (Bunda), Halima Bulembo (Muheza) na Peter Lijualikali (Nkasi).
Social Plugin