Serikali ya Tanzania imetangaza watumishi wapya 9,675 wa kada za elimu na afya walioajiriwa kufuatia kibali cha ajira kilichotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, Aprili, 2021.
Majina ya walimu waliopangiwa vituo vya kazi yanapatikana katika tovuti ya ofisi ya Rais-Tamisemi ya www.tamisemi.go.tz
Watumishi hao wapya wametangazwa na katibu mkuu ofisi ya rais Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe.
Profesa Shemdoe ametangaza ajira za elimu 6,749 kwa shule za msingi na sekondari na wataalamu wa afya 2,726.
Amesema waombaji wa kada ya ualimu walikuwa 99,583 na wataalam 37,437 wa kada ya afya wakiwemo wenye ulemavu 1,099 waliomba nafasi hizo.
“Baada ya kukamilisha taratibu zote za uchakataji wa maombi walimu 6,949 (3,949 wa shule za msingi na 3,000 wa shule za sekondari) na wataalam wa kada za afya 2,726 wamepangiwa vituo vya kazi,” amesema Profesa Shemdoe
Kuona Orodha ya Walimu Bofya hapa posted-applicants - 2021-06-25.pdf
Kuona Orodha ya Kada ya Afya Bofya hapa ORODHA YA WATUMISHI WA AJIRA MPYA KADA YA AFYA 25 JUNI, 2021.pdf