Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri wa Afya, Dk Dorothy Gwajima kuweka mpango mzuri wa ndugu kulipa deni la hospitali ili ikitokea mgonjwa wao amefariki dunia wakati akitibiwa, maiti isizuiwe.
Amesema utaratibu wa sasa ambao umekuwa ukizuia kutoa maiti hospitalini kwa kigezo cha kulipa gharama za matibabu kabla ya kifo si mzuri.
Rais Samià Suluhu Hassan ametoa agizo hilo jijini Dodoma wakati wa mkutamo wake na Wanawake wa Tanzania kupitia Wanawake wa mkoa wa Dodoma.
Amesema ni vema wakati wa matibabu ndugu wa mgonjwa ama mgonjwa mwenyewe akawa anapatiwa gharama za matibabu za kila siku, badala ya kusubiri hadi kifo kinapotokea, na hivyo kuleta usumbufu.
Social Plugin