Askari polisi aliyejulikana kwa jina la Amimu Abdalah Muzo (30) wa wilaya ya Shinyanga Mjini, mkazi wa Matanda Shinyanga amefariki dunia baada ya kugongwa na Basi la Allys akiendesha pikipiki katika eneo la Ibinzamata Barabara ya Shinyanga - Tinde.
Tukio hilo limetokea leo Ijumaa Juni 11,2021 saa mbili na nusu asubuhi wakati gari hilo lenye namba T.895 DMJ aina ya Dragon Bus kampuni ya Allys Star likielekea Kitup cha Mabasi lilimgonga mwendesha pikipiki yenye namba MC.272 cha aina ya SANLG , askari polisi aitwaye Amimu Abdalah Muzo na kusababishia kifo chake papo hapo.
Inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari aliyekuwa anatoka barabara kuu kwenda barabara ndogo bila kuchukua tahadhari na kusababisha mwendesha pikipiki huyo kugonga gari ubavuni kwa nyuma na kudondoka na kuingia chini ya uvungu wa gari na kukanyagwa na gari hiyo.
Taarifa zinaeleza kuwa dereva wa gari amekamatwa na gari husika lipo katika kituo cha polisi.
Social Plugin