Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BENKI YA CRDB, NHIF & KACU WATIA SAINI YA MAKUBALIANO YA BIMA ZA AFYA KWA WAKULIMA


Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) , Emmanuel Cherehani (kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt.  Joseph Witts (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya NHIF Hipoliti Lelo wakionesha nyaraka baada ya kutia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
***
 Na Kadama Malunde na Mavala - Kahama
Mkuu wa Wilaya Kahama Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya Bima ya afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB,NHIF na Chama Kikuu Cha Ushirika Kahama (KACU)

Akizungumza wakati wa utiaji saini huo leo Jumatatu Juni 7,2021 Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts amesema Benki ya CRDB imeamua kuwashika mkono wakulima kwa kuwalipia gharama zote zinazohusu huduma za afya na mkulima atalipia pindi atakapovuna mazao yake.

"Kupitia Mpango huu unaolenga kurahisha huduma za bima ya afya kwa wakulima, baada ya mavuno mkulima atarejesha malipo hayo bila riba yoyote baada ya kuuza mazao yao ambapo tunaanza kuwapatia bima ya afya Wakulima 590 wa tumbaku na wakulima 6800 wa pamba, jumla wakulima 7390", amesema Dkt.Witts.

"Mkulima akiwa anadunduliza anaweka kidogo kidogo katika benki yetu ya CRDB fedha zitakaa vile vile bila makato hata ya shilingi moja", ameongeza Dkt. Witts.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya NHIF Bw. Hipoliti Lelo amesema licha ya NHIF kuwa na jukumu la kuwafuata wanachama kukusanya michango na kuwapa matibabu wameamua kuwarahisishia wateja wao kwa kuwapa njia rahisi ya kulipa michango yao akibainisha kuwa ukiwa na Bima itagharamia matibabu ya familia nzima.

Kaimu Mrajisi wa Mkoa wa Shinyanga Hilda Boniface amewapongeza benki ya CRDB na NHIF kwa huduma hiyo huku akisisitiza kuwa kumekuwa na changamoto za wakulima wa tumbaku katika ulipaji wa mikopo kwa kuwa NHIF baada ya kutoa huduma isije ikawa kilio kwa Benki ya CRDB.

"Tuweke mikakati mizuri namna mikopo itavyolipwa ili isije ikawa mzigo kwa Benki ya CRDB", amesema Hilda.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Emmanuel Cherehani ameeleza kufurahishwa na hatua zilizochukuliwa na Benki ya CRDB na NHIF katika kusaidia wakulima na kuahidi kuwa atatoa ushirikiano wa hali ya juu ili kufanikisha adhma ya mkulima kupata matibabu na kulipa malipo taratibu na bila shida yoyote.

"Wakulima wote watakaokuwa wameandikishwa kwenye mfuko huu tuhakikishe wana uwezo mzuri wenye kilimo kikubwa na kidogo ili tuwavute wengi" ,amesema Cherehani.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Kahama Mhe. Anamringi Macha amesema moja ya changamoto kubwa katika wilaya ya Kahama ni hamasa na uelewa wa wananchi kujiunga na bima ya Afya akibainisha kuwa kama mkuu wa wilaya amekuwa akipiga kampeni kubwa ili kuhakikisha wananchi wanajiunga na bima ya afya kitu ambacho ni kizuri na kinapunguza gharama za matibabu pindi wana familia wanapoumwa.

Licha ya kuwapongeza CRDB,NHIF na KACU amewaomba waendelee kutoa hamasa kwa wananchi wajiunge na huduma za afya.

"Kwa mazingira ya sasa magonjwa ni mengi na gharama za matibabu ni kubwa kwa hiyo suala la kuwa na Bima ni muhimu sana. Naomba viongozi tuendelee kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya kwani wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakipotosha kuhusu huduma za afya kitu ambacho kinapelekea wananchi kutokuwa na maamuzi sahihi," amesema Macha.
Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt.  Joseph Witts akitia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB,NHIF na KACU uliofanyika leo Jumatatu Juni 7,2021 Mjini Kahama
Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt.  Joseph Witts  (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya NHIF Hipoliti Lelo  wakitia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB,NHIF na KACU
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU), Emmanuel Cherehani akitia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU . Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akishuhudia utiaji saini
Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt.  Joseph Witts akibadilisha nyaraka na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya NHIF Hipoliti Lelo wakati wa kutia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) , Emmanuel Cherehani (kushoto) akibadilishana nyaraka na Mkurugenzi mkuu wa biashara Benki ya CRDB, Dkt.  Joseph Witts wakati wa kutia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Bwana Emmanuel Cherehani (kushoto) akibadilishana nyaraka na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya NHIF Hipoliti Lelo wakati wa kutia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) , Emmanuel Cherehani (kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt.  Joseph Witts  (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya NHIF Hipoliti Lelo wakionesha nyaraka baada ya kutia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa utiaji saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Kaimu Mrajisi mkoa wa Shinyanga Hilda Boniface akizungumza wakati wa utiaji saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Mkurugenzi mkuu wa biashara Benki ya CRDB, Dkt.  Joseph Witts  akizungumza wakati wa utiaji saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya NHIF Hipoliti Lelo akielezea umuhimu wa bima ya afya wakati wa utiaji saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Bwana Emmanuel Cherehani akizungumza wakati wa utiaji saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Mkuu wa Wilaya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (katikati) akiwa na viongozi wa Benki ya CRDB,NHIF na KACU katika hafla ya utiaji saini makubalinao ya Bima ya afya kwa wakulima kati ya benki ya CRDB,NHIF na KACU
Mkuu wa Wilaya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ,viongozi wa Benki ya CRDB,NHIF na KACU pamoja na wadau wa kilimo wakipiga picha ya kumbukumbu
Mkuu wa Wilaya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ,viongozi wa Benki ya CRDB,NHIF na KACU pamoja na wadau wa kilimo wakipiga picha ya kumbukumbu
Mkuu wa Wilaya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ,viongozi wa Benki ya CRDB,NHIF na KACU pamoja na wadau wa kilimo wakipiga picha ya kumbukumbu


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com