Mama mmoja kutoka eneo la Masinga nchini Kenya amejuta baada ya kunaswa na mkazamwana (mke wa mwanae/mwinga) usiku wa manane akimtorosha mwanawe (mjukuu) kumshirikisha katika vituko vya ushirikina.
Inasemekana kuwa mama huyo aliponea kichapo cha wanakijiji wenye ghadhabu ambao walimlaumu kwa kuendeleza ushirikina.
Kwa mujibu wa Taifa Leo, mama alimchukua mjukuu wake wa umri wa miaka sita usiku wa manane na kutoka naye nje ya nyumba.
Inaarifiwa kuwa kwa bahati nzuri mamaake mtoto huyo aligutuka kutoka usingizini na kumkabili mama kabla ya kutokomea gizani katika kichaka cha karibu na eneo hilo.
“Wampeleka wapi mwanangu usiku wa manane wakati watu wamelala? Kwani umepanga kumtoa mwanangu kafara wewe?” mama watoto aliuliza.
Penyenye zinasema kuwa mke wa mwana wa mama huyo na mtoto wake walikuwa wamefika nyumbani kutoka jijini.
Mvulana huyo kwa muda mrefu alikuwa akimsihi mamaake ampelekea kumwona nyanyake/bibi lakini wasilojua ni kwamba ajuza huyo alikuwa muovu.
“Sema ulikotoka kumpeleka mwanangu, la sivyo, nitawaomba wanakijiji tushirikiane tukutie moyo,” mama wa mtoto alitisha. Hapo ndipo alipobaini wanakijiji walikuwa wakimshuku mama huyo pia.
“Lo! Kumbe isemwavyo ni kweli! Huyu Bi Kizee amekuwa mwiba hapa kijijini. Kumbe hata hana huruma na mjuku wake?” alishangaa mama mmoja.
“Anasifika kwa mazingaombwe na si ajabu kumdhuru mjukuu wake,” mzee mwengine alisema. “Basi, nioneeni huruma. Nitausema ukweli. Mimi ni mchawi. Nilipanga kumtibu mjukuu wangu asirogwe,” alikiri mbele ya watu wote.
“Nimecheshwa na tabia zangu hizi za kishetani. Nisameheni nami naapa sitawahi kuzifanya tena. Natamani kuishi nimpendeze Mungu pekee,” ajuza aliomba radhi. Wanakijiji wenye ghadhabu walimsamehe ila wakamwonya kwamba iwapo atapatikana tena siku nyingine, atakiona cha mtema kuni.
Chanzo - Tuko News
Social Plugin