Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ndg Daniel Chongolo akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali wa Jumuiya na chama akikata Utepe kuashiria kuzindua Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo Chuo cha Mafunzo Ihemi Iringa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Daniel Chongolo akizungumza, wakati wa akifungua Mafunzo ya Wenyeviti wa UVCCM Nchi Nzima uliofanyika katika Chuo Cha Mafunzo Ihemi Mkoani Iringa, leo tarehe 19 Juni 2021
Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka ,Akizungumza , wakati wa tukio la ufunguzi wa Mafunzo ya Wenyeviti wa UVCCM Nchi Nzima uliofanyika katika Chuo Cha Mafunzo Ihemi Mkoani Iringa ,leo tarehe 19 Juni 2021
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Kheri James (MCC) , wakati wa tukio la ufunguzi wa Mafunzo ya Wenyeviti wa UVCCM Nchi Nzima uliofanyika katika Chuo Cha Mafunzo Ihemi Mkoani Iringa ,leo tarehe 19 Juni 2021
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg Salim Asasi Akizungumza , wakati wa tukio la ufunguzi wa Mafunzo ya Wenyeviti wa UVCCM Nchi Nzima uliofanyika katika Chuo Cha Mafunzo Ihemi Mkoani Iringa ,leo tarehe 19 Juni 2021
Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi na mkufunzi wa Mafunzo hayoNdg Zacharia Mwasasu akifuatilia baadhi ya nyaraka za mafunzo hayo
katibu Mkuu wa CCM Ndg Daniel Chongolo (kulia) akifurahi jambo na Mwenyekiti wa UVCCM Ndg Kheri James pamoja na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Ndg Salim Abri Asasi, wakati wa tukio la ufunguzi wa Mafunzo ya Wenyeviti wa UVCCM Nchi Nzima uliofanyika katika Chuo Cha Mafunzo Ihemi Mkoani Iringa ,leo tarehe 19 Juni 2021
Katibu Mkuu wa UVCCM Komred Raymond Mwangwala akizungumza , wakati wa tukio la ufunguzi wa Mafunzo ya Wenyeviti wa UVCCM Nchi Nzima uliofanyika katika Chuo Cha Mafunzo Ihemi Mkoani Iringa ,leo tarehe 19 Juni 2021
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ndg Queen Sendiga akitoa Salamu za Mkoa wakati wa tukio la ufunguzi wa Mafunzo ya Wenyeviti wa UVCCM Nchi Nzima uliofanyika katika Chuo Cha Mafunzo Ihemi Mkoani Iringa ,leo tarehe 19 Juni 2021
Meza Kuu ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ,Ndg Daniel Chongolo (Tatu toka kulia),Shaka Hamdu Shaka ,Katibu wa H/Kuu Itikadi na Uenezi (Kwanza Kulia),Mwenyekiti wa UVCCM Komred Kheri James,(wa nne Kulia), Mjumbe wa H/Kuu ya CCM Ndg Salim Asasi (wa tano kulia) ,Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg Raymond Mwangwal (wa kwanza kushoto), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Ndg Abel Nyamahanga (wa Pili Kulia) pamoja Mkuu ,leo tarehe 19 Juni 2021
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ndg Daniel Chongolo akipanda Mti wa Kumbukumbu Katika eneo la Chuo cha Mafunzo Ihemi Iringa,leo tarehe 19 June 2021
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ndg Daniel Chongolo akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali wa Jumuiya na chama akikata Utepe kuashiria kuzindua Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo Chuo cha Mafunzo Ihemi Iringa.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ndg Daniel Chongolo (wa pili kulia) akipewa maelezo na Katibu Mkuu wa UVCCM Komred Raymond Mwangwala wakati akikagua eneo la nje ya Ukumbi wa Benjamin Mkapa kabla ya Kuuzindua ukumbi huo ,Katika Chuo cha Mafunzo Ihemi Iringa.
....................................................................................
Katibu mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo leo amezindua ukumbi wa Benjamini Mkapa katika chuo cha mafuzo cha umoja wa vijana CCM Ihemi mkoani Iringa pamoja na kufungua mafunzo ya wenyeviti wa wilaya wa umoja wa vijana.
Ndg. Chongolo amewataka Viongozi hao kuendelea kulinda taswira ya chama cha mapinduzi na viongozi wake kwani hilo ndio jukumu kubwa la kiundwa kwa jumuiya hiyoo.
"Chama hiki akina mtu wa kukilinda isipokuwa Vijana, tuna wajibu na tumehapa kulinda Heshima ya Viongozi wetu, tunao wajibu mkubwa wa kulinda Mhe. Rais wetu na mwenyekiti wa chama chetu Samia Suluhu Hassan", amesema.
Aidha Ndg. Katibu mkuu Chongolo ametoa maelekezo kwa Viongozi hao kuendelea kukaa na kutafakari namna ambavyo watachochea nguvu na maarifa yao kwa chama mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
Pamoja na hayo Ndg. Chongolo ameeleza kuwa nafasi ya vijana katika taifa lolote duniani ni kubwa hivyo wanategemewa katika ujenzi wa uchumi na Maendeleo ya Taifa.
Pamoja na Mambo mengine Ndugu Chongolo ameshukuru Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na imani kubwa kwa vijana na kumteua yeye katika nafasi hiyo kubwa kutoka kwenye kundi la vijana.
Katika tukio hilo Ndugu Katibu Mkuu aliambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka H. Shaka
Social Plugin