Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAMAA MATATANI BAADA YA KUNASWA LIVE AKIPAKUA ASALI YA JIRANI YAKE...AAMRISHWA ACHANGIE MAHARI

Jamaa mmoja kutoka eneo la Seme, Kisumu nchini Kenya amejikuta pabaya na kulazimishwa kuchangia mahari baada ya kunaswa peupe akipakua asali kutoka kwa mzinga wa jirani yake. 

Penyenye zinasema kuwa jamaa amenaswa akila uroda na mke wa jirani ambaye alipowasili nyumbani na kugundua kilichokuwa kikiendelea alifunga mlango kwa nje kumzuia mshukiwa kuponyoka.

“Jamani leo nimeshika. Njooni muone,” mwenye nyumba alipiga mayowe kuwaita watu kulingana na Taifa Leo. 

Punde si punde boma lilifurika watu. “Jirani yangu yumo ndani. Nimempata hadharani kitandani na mke wangu,” jamaa alieleza.

 Duru zinaarifu kwamba umati huo ulichacha kwa hasira na kumtaka jamaa afungue mlango ili wampe kichapo mwizi huyo wa mapenzi.

 “Sifungui mlango. Nawasubiri wazee waje kisha waamue hii kesi,” jamaa alidai.

Muda mfupi baadaye wazee waliwasili naye mwenye nyumba akawaeleza kila kitu.

Baada ya wazee kutulia mlango ulifunguliwa. Mara tu mlango huo ulipofunguliwa wanaume waliokuwa wamefika bomani humo kujionea kisanga hicho walimrukia na kuanza kumzaba jirani huyo makofi.

 “Huyu ni jirani yangu. Nimekuwa nikishuku kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mke wangu,” jamaa aliwaarifu wazee. Inasemekana kimya kilitawala huku kila mmoja akitaka kupata uhondo.

“Nikiondoka kwa boma huwa napata habari kwamba mke wangu huonekana naye kila mahali, sio sokoni, sio wakitoka gesti fulani,” mwenye boma alisema huku vicheko vikishamiri.

“Leo nimempata mwenyewe juu ya mzinga. Kile ninataka wazee waamue ni kwamba achangie kulipa mahari kwa kuwa ni wazi tunachovya asali kutoka mzinga mmoja,” jamaa alisema.

 Penyenye zinasema kuwa jamaa alijaribu kuomba msamaha lakini hakuna aliyetaka kumsikia. 

“Hii tabia umekuwa ukiifanya kwa muda. Faini unayopigwa kwa sasa ni wewe kuchangia mahari. Mahari hayo unaitoa leo,” jamaa alifokewa huku akibaki mdomo wazi. 

“Ng’ombe watatu ambao umefuga walete sasa hivi,” kijogoo aliamrishwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com