Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAPTENI MSTAAFU GEORGE MKUCHIKA AAPISHWA KUWA WAZIRI KATIKA OFISI YA RAIS IKULU, KAZI MAALUM


Rais Samia Suluhu Hassan amemuapisha Kapteni Mstaafu George Mkuchika kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais Ikulu, Kazi Maalum.

Kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, Kapteni Mstaafu Mkuchika alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, nafasi inayoshikiliwa hivi sasa na Mohamed Mchengerwa.

Hafla ya kuapishwa kwa Kapteni Mstaafu Mkuchika imefanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, ambapo pia Makatibu Tawala wa mikoa walioteuliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan wameapishwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com