AFISA
Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga Buluba Kanuda
akieleza jambo wakati wa mkutano huo kulia ni Meneja wa Maendelea ya
Biashara wa Benki ya NBC Tanga Aljiran Mbwani
Meneja
wa Maendelea ya Biashara wa Benki ya NBC Tanga Aljiran Mbwani akieleza
jambo wakati wa mkutano huo kulia ni Afisa Biashara wa Jiji la Tanga
Sehemu ya Washiriki katika mkutano huo wakifuatilia kwa umakini
Sehemu ya Washiriki katika mkutano huo wakifuatilia kwa umakini
KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeeleza kwamba kila
nchi hata zile zilizoendelea duniani zinahitaji wawekazaji ambao
watawasaidia kuweza kukuza uchumi wao, pato la taifa, kuongeza mapato ya
kikodi na yasiyo ya kikodi, kuzalisha ajira hasa kwa vijana, kuingiza
teknolojia za kisasa, na kuongeza mitaji ya nje (FDI).
Hayo
yalisemwa na Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Kanda ya Kaskazini (TIC) Bw.
Daudi Riganda wakati wa mkutano uliolenga kuwaunganisha wawekezaji
wakubwa na wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs) uliofanyika katika
ukumbi wa VETA mjini Tanga.
“Kwetu
sisi Tanzania wawekezaji ni muhimu sana na hata nchi ambazo zimeendelea
nazo zinahitaji wawekezaji mfano ukienda Dubai, Uingereza, Brazil na
kwingine kote wawekezaji wanahitajika kwa sababu wana mchango mkubwa
katika ukuaji wa uchumi na ndio maana Rais wetu mpendwa mama Samia
Suluhu Hassan moja wapo ya agenda zake ni uwekezaji”, alisema.
“Lakini
nieleze kwamba kama uwekezaji hamna hata pato la Taifa litashuka hivyo
tunahitaji uwekezaji kwa ajili ya kutusaidia kupata mapato ya kikodi na
yasiyokuwa ya kikodi kwa sababu kupitia uwekezaji makampuni yatalipa
kodi na matokeo mengine mengi zikiwemo ajira kuonekana “, alisema Meneja
huyo.
Aliongeza kusema
“ikiwa sekta binafsi itakuwa dhaifu basi matokeo kama ajira, kodi,
teknolojia za kisasa nk pia yatapungua. Katika nchi zilizoendelea na
zinazoendelea duniani, sekta binafsi ndio injini ya maendeleo, na
uwekezaji muhimu unatoka sekta binafsi".
Awali
akizungumza katika mkutano huo, Meneja Utawala wa Kiwanda cha Maweni
Limestone Aron Mushi alikishukuru Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa
namna walivyowakutanisha na wajasiriamali na wadau wengine kuweza
kuangalia changamoto ambazo wanakutana nazo ili kufanya uwekezaji uweze
kukua, na wakati huo huo kusaidia ukuaji wa SMEs.
Alisema
pia wanashukuru kwa kupata fursa ya kueleza yanayowakabili na kuweza
kuishauri serikali kuona yale yanayofaa kwa ukuaji wa miradi yao na
uchumi wa nchi kwa ujumla.
Aidha,
kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Afri Line Tanga, Bi. Veronika John
aliishukuru TIC kwa hatua ya kuwakutanisha wao kama wajasiriamali na
wawekezaji kuongea nao na kuweza kujua changamoto wanazokumbana nazo kwa
namna moja au nyingine.
Alisema
kwa sababu wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs) wakati mwingine
wamekuwa wakilalamika kuhusu wawekezaji kumbe wao ndio chanzo cha
changamoto zinazowakabili na hivyo kushindwa kuwalipwa kwa wakati.
Hata
hivyo alitoa wito kwa SMEs kujaribu kufanya kazi kwa kupenda shughuli
au huduma wanazotoa ili kuweze kuwa endelevu kwa kuboresha ubora muda
hadi muda.
Social Plugin