Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya NBC Tanga Aljiran Mbwani akieleza jambo wakati wa mkutano huo kulia ni Afisa Biashara wa Jiji la Tanga
Sehemu ya Washiriki katika mkutano huo wakifuatilia kwa umakini
Sehemu ya Washiriki katika mkutano huo wakifuatilia kwa umakiniSehemu ya Washiriki katika mkutano huo wakifuatilia kwa umakini
KITUO cha uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanya mkutano Jijini Tanga uliolenga kuwaunganisha wawekezaji wakubwa na wajasiriamali wadogo na wakati (SMEs)
Mkutano huo wa siku tatu ulililenga kufanya utafiti na kuwajengezea uwezo wawekezaji wakubwa na wajasiriamali wanaotoa huduma na bidhaa mbalimbali kwa wawekezaji hao.
Akizungumza katika mkutano huo Meneja wa Kituo cha Uwekezaji (TIC ) Kanda ya Kaskazini, Bw. Daudi Riganda alisema katika kutekeleza hilo waliweza kuanisha bidhaa na huduma za wajasiriamali ambazo wawekezaji wakubwa wanaweza kuzitumia Kuainisha wajasiriamali wanaoweza kusambaza bidhaa na huduma kwa wawekezaji ikiwemo kubainisha wawekezaji ambao wanaweza kutumia bidhaa na huduma za wajasiriamali.
Alisema kwa kutambua changamato zinazokwamisha wajasiriamali kutoa huduma na bidhaa bora kwa wawekezaji na kuwa jengea uwezo wajasiriamali na kisha kuwaunganisha na taasisi za fedha.
Aidha alisema jumla ya makampuni makubwa manne (4) ya wawekezaji yaliweza kushirikishwa kwenye zoezi hili lililofanyika katika ukumbi wa VETA jijini Tanga kuanzia Juni 16 hadi Juni 18 mwaka huu.
Aliyataja makampuni hayo kuwa ni Tanga Cement PLC (wazalishajiwasarujiya Simba), Maweni Limestone Limited (wazalishaji wa chokaa na “clinker”), Tanga Fesh Limited (wazalishaji wa maziwa), Pee Pee Tanzania Limited (wazalishaji wa aina mbalimbali za mifuko ya kufungia bidhaa).
Aidha alisema pia wajasiriamali kumi tano (15) waliweza kushirikishwa katika zoezi hili kutoka kwa watoa huduma na bidhaa mbalimbali kama vile usafirishaji, ulinzi, chakula, wafugaji wa ng’ombe wa maziwa, n.kmkoaniTanga.
Akizungumzia baadhi ya mapungufu ya wajasiriamali yaliyobainishwa na wawekezaji katika kutoa huduma na bidhaa mbalimbali alisema ni pamoja na huduma au bidhaa kutokuwa na ubora, wajasiriamali kutokujisajili kama walipa kodi (kutokuwa na TIN),kuchelewa kutoa huduma/bidhaa kama mkataba unavyowataka, bidhaa kutegemea msimu, uwezo/ufanisi mdogo wa wajasiriamali, nk.
Hata hivyo alisema wajasiriamali wenyewe wamelalamikia uhaba wa masoko kwa bidhaa/hudumazao, kuchelewa kulipwa na makampuni ya wawekezaji baada ya kutoa huduma/bidhaa, kukosekana kwa mitaji, riba zinazotozwa na mabenki kuwa kubwa, n.k.
Mbali na wawekezaji na wajasiriamali, mkutano huu uliwashirikisha pia wawakilishi wa baadhi ya taasisi za serikali kama vile jiji la Tanga lililowakilishwa na Afisa Biashara wake, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), VETA, na wawakilishi kutoka taasisi za fedha kama NMB Benki, CRDB Benki na NBC Benki.
Akizungumza wakati wa kufunga Mkutano huu, Meneja Riganda aliwaasa wawekezaji na wajasiriamali kuheshimu mikataba wanayoingia pande mbili katika kutoa na kupokea huduma/bidhaa mbalimbali za wajasiriamali huku akiwataka wajasiriamali kuzingatia ubora wakati wa utoaji wahuduma/bidhaa zao na taasisi za fedha kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wawekezaji.
Aidha alitoa rai kwa taasisi za serikali kushirikiana katika kutengeneza mazingira ya biashara na uwekezaji yatakayomsaidia mjasiriamali kukua ili siku moja mjasiriamali huyo awe mwekezaji.
Katika Mkutano huo Kituo cha Uwekezaji Makao Makuu kiliwakilishwa na Bi. Phina Lyimo ambaye ni Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Utafiti.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania ni taasisi ya umma iliyoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 26 ya mwaka 1997 kwa ajili ya kuratibu masuala ya uwekezaji nchini, kuhamasisha uwekezaji, kuvutia uwekezaji, kusaidia/kufanikisha uwekezaji nchini na kuishauri serikali kuhusu masuala ya mazingira ya uwekezaji na sera hapa nchini.
Utekelezaji wa mkutano huu uliolenga kuwaunganisha wawekezaji na wajasiriamali kibiashara unatokana na Lengo F la Kimkakati la Kituo linalokitaka Kituo hicho kufanya shughuli zinazolenga kusaidia maendeleo ya wajasiriamali wadogo na wakati (SMEs) hapa nchini.
Social Plugin