Na Lucas Raphael,Tabora
Wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi mkoa waTabora kwa kushirikiana na kanda ya kati inazidai Taasisi serikali na watu binafsi wakiwemo wananchi kiasi cha shilingi bilioni 3.1 kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita
Afisa mipango mwandamizi na mratibu wa kodi kanda ya kati ,Tatu Simba akizungumza katika mkutano wa hadhara ulifanyika katika kata ya Isevya manispaa ya tabora kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kulipa kodi ya ardhi na pango la ardhi.
Alisema kwamba kumekuwepo na malimbikizoya ya madeni ya kodi ya Ardhi na pango la ardhi mkoani Tabora na wilaya zake 7 kiasi cha shilingi bilioni 3.140.673.812 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2017 hadi 2021.
“Hali hiyo inachangia kuzorotesha kwa pato la nchi ambalo ni msingi wa maendeleo na ustawi wa watanzania nakuchelewesha maendeleo ya nchi”.alisema Tatu.
Hata hivyo afisa huyo alizitaka Taasisi binafsi zenye madeni sugu kulipa madeni yao kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa ili kufanikisha malengo endelevu ya nchi.
Aidha aliendelea kusema kwamba “kama yupo mwananchi mlipa kodi ya ya ardhi na pango anapata tabu katika kujua viwango vya kodi ardhi au pango ambayo amekadiriwa afike ofisi za kamishna msaidizi wa mkoa ili apewe tozo sahihi aweze kulipa”.alisema Tatu Simba
Hata hivyo wananchi hao walitaka kupata kufafanuzi na tofauti kati ya kodi ya ardhi na kodi ya pango la ardhi alitolea ufafanuzi huo
Akitoa ufafanuzi huo mratibu wa kodi mkoa wa Tabora Evody Krety alisema kodi ya ardhi ni tofauti na kodi ya pangpo la nyumba anakuongeza kuwa kodi ya pango la ardhi linalipwa kwa ajili ya umiliki wa ardhi
mwisho