MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AWASILI NCHINI UFARANSA KUHUDHURIA JUKWAA LA KIZAZI CHENYE USAWA
Wednesday, June 30, 2021
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango Juni 29, 2021 amewasili Paris nchini Ufaransa ambako atahudhuria Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum) linalofanyika Paris Ufaransa kuanzia Juni 30 – Julai 2, 202. Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa hilo.
Aidha, Makamu wa Rais alipata maelezo jinsi Ubalozi wa Tnazania unavyotekeleza Sera ya Diplomasia ya Uchumi katika eneo lake uwakilishi ambalo ni Ufaransa, Hispania; Ureno; Algeria na Morocco. Maelezo hayo yalitolewa na Mhe. Samwel Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Pia Balozi Shelukindo anaiwakilisha Tanzania katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango amempongeza Balozi Shelukindo kwa uwakilishi mzuri katika nchi hizo na kumuhakikishia serikali itaendelea kutatua changamoto zinazojitokeza katika ubalozi huo. Amemtaka kuendelea kutafuta mahusiano na sekta binafsi zilizopo nchini Ufaransa kwa manufaa ya nchi zote mbili. Hapo kesho juni 30,2021 Makamu wa Rais anatarajia Kuhudhuria ufunguzi wa Jukwaa la kizazi cha usawa lenye lengo la kuchagiza haki za usawa wa kijinsia kama zilivyokubaliwa katika mkutano wa Beijing wa mwaka 1995.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin