Dk Chrisant Majiyatanga Mzindakaya enzi za uhai wake
Na Walter Mguluchuma KTPC,Sumbawanga.
Taarifa za simanzi za kifo cha mwanasiasa mkongwe nchini,Dk Chrisant Majiyatanga Mzindakaya (80) sio tu zimeacha simanzi hapa nchini,bali pia zimewagusa kwa namna ya kipekee wakazi wa mkoa wa Rukwa.
Akizungumza kwa njia ya simu mdogo wake na Marehemu Dk Mzindakaya,Meja Mstaafu wa JWTZ, Christopher Mzindakaya alisema maziko yake yanatarajiwa kufanyika Juni,09 mwaka huu.
Dk Mzindakaya ambaye alifikwa na umati Juni 7 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Jijini Dar es Salaam alikokuwa akitibiwa ambapo maziko yake yatafanyika katika makazi yake yaliyopo katika eneo la Kilimani nje kidogo ya Mji wa Sumbawanga.
Aliongezakuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo ambapo awali alilazwa katika Hospitali ya Agha Khan iliyopo katika Jiji la Dar -Es - Salaam kabla ya kuhamishiwa MNH hadi umauti ulipomfikia.
"Familia tumeupokea msiba huu kwa masikitiko makubwa ameacha pengo kubwa kwetu alikuwa mshauri mkubwa wa familia ...mwezi mmoja uliopita akijiandaa kwenda kutibiwa alipita hapa nyumbani kwangu kumuaga ilikuwa kama alikuja kuniaga" alisema kwa simanzi kubwa.
Licha ya kuwa ni mwanasiasa mkongwe nchini pia alikuwa mjasiriamali wa mfano,mzee wa kimila na mcha Mungu.
Alizaliwa Desemba 31,1940 mkoani Rukwa.
Alijiunga na Shule ya Sekondari Bugerere nchini Uganda katika ya 1960-1961, mwaka 1963-1964 alijiunga na Chuo cha Maendeleo ya Jamii,Tengeru mkoani Arusha kwa ngazi ya cheti.
Baada ya hapo alikuwa Ofisa Maendeleo Msaidizi Wilaya ya Sumbawanga.
Alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Biashara ya Ndani (BIT) katika ya 1973-1975 ambapo 1975- 1987 alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwanda Vidogo nchini (SIDO),1969-175 alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Tanu" TANU Youth League).
1992 alikwenda masomoni Dublin nchini Ireland kusomea mafunzo ya Utawala na Mipango ya Maendeleo kwa ngazi ya cheti.
1990- 1992 alikuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Rukwa,1990- 1997 alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na mbunge kwa kipindi kirefu.
CHANZO - KATAVI PRESS CLUB BLOG