Mhubiri na mwanzilishi wa kanisa la Deeper Christian Life Ministries Williams Folorunsho Kumuyi amewaonya waumini wake dhidi ya kutoa zaka na sadaka iwapo wao ni watenda dhambi.
Mhubiri huyo alitishia kuwarejeshea zaka na sadaka waumini wote ambao atagundua kwamba ni watenda dhambi.
Kulingana na mhubiri huyo kuishi katika utakatifu ni muhimu kuliko kusaidia kanisa kupitia kwa sadaka na zaka.
Aidha, Mhubiri huyo alikuwa anasisitiza kuhusu umuhimu wa kuishi maisha ya utakatifu, na kumtolea Mungu sadaka inayomfurahisha.
Kulingana na mhubiri huyo, hakuna kiwango cha sadaka hata kiwe kikubwa kivipi kinaweza kushinda utakatifu katika binadamu.
Mhubiri huyo aliongezea kwamba wale ambao wanatoa rasilimali zao kwa ajili ya kusaidia kanisa lakini wanaendelea kuwa kwenye dhambi, wanapoteza tu muda na rasilimali zao.
Kwa mtazamo wake Kumuyu alisisitiza kwamba Mungu hahitaji fedha kutoka kwa wenye dhambi, aliwashauri waumini wabadili mwenendo iwapo kuna kati yao katika kanisa lake.
"Kama kuna yule anawajua wale wamekuwa wakitoa zaka na sadaka na wamekuwa wakifanya dhambi, naomba nipewe orodha ya majina yao, niko tayari kuwarejeshea sadaka yao," Alisema Mhubiri Kumuyi.
Aidha, madai hayo yalibua maoni tofauti kutoka kwa wanamitandao, wengi wakidai hakuna mtu mkamilifu duniani asiyekosa dhambi.
Chanzo - Tuko News
Social Plugin