Mwanafunzi Josephat John, aliyekuwa anasoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kom iliyopo Manispaa ya Shinyanga, amezua taharuki ya aina yake leo mchana Ijumaa Juni 4,2021 mjini Shinyanga mara baada ya kujianika juani huku akiwa amevaa mabango na kujifunika maboksi yenye ujumbe wa kupinga kuchaguliwa masomo ya Economics, Commerce , Accounts (ECA) ambayo amedai hawajawahi kuyasomea kwani yeye amesomea masomo ya Physics, Chemistry, Biology (PCB).
Ametumia mbinu hiyo ya kuvaa mabango kuiomba Wizara husika ifanye uchaguzi upya wa michepuo ili akasomee masomo ambayo ameshayasoma.
Tukio hili limekuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu atangaze matokeo ya wanafunzi waliochaguliwa kwenda vyuo vya ufundi na vyuo vya kati na kidato cha Tano mwaka 2021.
Mwanafunzi Josephat John, aliyekuwa anasoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kom iliyopo Manispaa ya Shinyanga, akiwa amevaa mabango na kujifunika maboksi yenye ujumbe wa kupinga kuchaguliwa masomo ya Economics, Commerce , Accounts (ECA) ambayo amedai hawajawahi kuyasomea kwani yeye amesomea masomo ya Physics, Chemistry, Biology (PCB). Picha na Malunde 1 blog