NAIBU WAZIRI CHANDE ATEMBELA KORONGO LA SHABANI ROBERT WILAYANI MPWAPWA


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Hassan Chande, amefanya ziara katika korongo la Shabani Robert Wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma, kujionea athari zinazojitokeza kutokana na mabadiliko ya tabianchi.


Aidha Mhe. Chande amesema kuwa serikali ipo pamoja na wananchi katika kupambana na changamoto zinazojitokeza kutokana na mabadiliko ya Tabianchi na kupelekea kuongezeka kwa korongo ambalo linaleta athari kubwa. Amesema kuwa athari hizi zinajitokeza kutokana na uharibifu wa mazingira hivyo amewataka wananchi kutunza na kuhifadhi mazingira ili kuepusha madhara hayo


"Lengo la kuja hapa ni  kujionea korongo la Shabani Robert ambalo linatanuka kutokana na  mvua hivyo kupelekea athari kwa wananchi na mpaka baadhi ya wananchi kupoteza uhai pamoja na mali zao, takribani makazi ya kaya 29 pamoja na watu sita wamepoteza maisha yao kutokana na korongo hili, hivyo serikali halitalifumbia macho niwatoe hofu wanampwapwa serikali  inajipanga kushughulikia suala hili".


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir shekimweli, amesema kuwa kuna changamoto nyingi zinawakabili hasa kipindi cha mvua maana mvua zinazokuja zinakuwa nyingi ambazo zinasababisha baadhi ya madaraja kukatika, hivyo ningeomba serikali Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo ni Wizara inayohusika na masuala ya mazingira kusaidia  ili kuweka kingo katika korongo hilo ili kuepusha athari hizo.


Vile vile Mhe.George Malima ambae ni mbunge wa Mpwapwa, amesema ana imani kubwa sana na serikali hii na anaamini changamoto zinazojitokeza katika Wilaya ya Mpwapwa itapata suluhu na maisha ya wananchi hao yatakuwa salama. Amesema maisha ya watu yapo hatarini na ili kuweza kutatua changamoto hizi serikali kuu inahitaji kuwekeza nguvu ya ziada kwani Halmashauri pekee haiwezi.


Kwa upande wake Bi. Rukia Ally Msonga ambaye ni Mwananchi, ameomba serikali kuwapa msaada ili waweze kuishi kwa amani amesema kama serikali itawapendeza watafute suluhu ya changamoto hiyo kwani korongo hilo hapo zamani lilikuwa dogo sana lakini siku zinavyozidi kwendwa linazidi kukua na kufata makazi ya watu


Mhe.Chande amesema kuwa changamoto hizo wamezipokea na suluhu itapatikana hivi karibuni lakini ameiagiza Halmashauri ya Mpwapwa kusimamia na kuhakikisha wanakuwa na sehemu ya kutupia taka na wananchi waache mara moja kutupa taka katika korongo hilo kwani unapotupa taka uchafuzi na uharibifu wa mazingira unaendelea na athari zinaongezeka




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post