Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : MAADHIMISHO YA SIKU YA BABA DUNIANI YAFANYIKA KWA MARA YA KWANZA TANZANIA...NACOPHA YASHIRIKI, KATAMBI AFUNGUKA AKIWA NA MTOTO MGONGONI

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akizungumza huku amebeba mtoto mgongoni ikiwa ni ishara ya kuunga mkono shughuli zinazofanywa na wanawake katika familia kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ameongoza Maadhimisho ya Siku ya Baba Duniani ‘Father’s Day’ kitaifa ambapo kwa mara ya kwanza yamefanyika nchini Tanzania katika mkoa wa Shinyanga.

Maadhimisho ya Siku ya Baba Duniani nchini Tanzania yamefanyika leo Jumapili Juni 20,2021 yamefanyika katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga  yakiongozwa na Kauli Mbiu ‘Tembea katika viatu vyake, thamini mapambano yake’.

Maadhimisho hayo ya Siku ya Baba Duniani yenye lengo la kusherehekea michango ya baba kwenye maisha ya watoto na familia kwa ujumla yaliyoanza mwaka 1910 nchini Marekani yameandaliwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau likiwemo Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) na ICS Africa.

Katika maadhimisho hayo, wababa wameonesha kwa vitendo baadhi ya shughuli zinazofanywa na wanawake ili kuonesha namna baba bora anavyoshirikiana na mke wake katika majukumu ya matunzo,malezi na makuzi ya familia na watoto. Pia kumefanyika zoezi la kuchangia damu salama na kupima afya huku maandamano na burudani mbalimbali zikinogesha maadhimisho.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi amesema mkoa wa Shinyanga umeamua kutumia siku ya Baba Duniani kuwapa wanaume nafasi  ya kutumia katika kulinda usalama wa wanawake na watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia kama watetezi wa haki za binadamu na walinzi wakuu wa familia na jamii.

“Lengo la siku hii ni kuwafanya wanaume kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia,maadhimisho haya yamekusudia kutambua mchango wa wababa kama viongozi wa familia kwa kuwa wana wajibu mkubwa wa kulinda, kutunza,kuongoza na kustawisha familia katika Nyanja za kijamii,kielimu,kiuchumi na kiroho”,ameongeza Katambi.

Amesema maadhimisho ya siku ya Baba duniani yatakuwa chachu kwa wababa wa mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla katika kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto lakini pia kutambua mchango wa baba bora, baba anayejali na kuheshimu utu wa wanawake, wasichana na watoto.

Katika hatua nyingine, Katambi ametumia fursa hiyo kulipongeza Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA)  kwa kuwa mstari wa mbele katika shughuli za mwitikio wa UKIMWI sambamba na kupinga vitendo vya unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na VVU pamoja na kutetea maslahi ya watu wanaoishi na VVU nchini.

“Ni dhambi na ni marufuku kumcheka na kunyanyapaa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU ama mtu mwenye ulemavu kwani hakuna ajuaye kesho yake. Waliopata maambukizi hawakupenda. Tupendane, tuwe wamoja na tushirikiane. Naomba wanaume tuwe mstari wa mbele kupima afya zetu na tukibainika tumepata maambukizi basi tuanze kupata huduma ya dawa”,amesema Katambi.

Katambi amewataka wababa kutambua changamoto wanazopitia wake zao na kuwathamini hivyo kutoa wito kwa wababa wote kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanashirikiana na wake zao katika majukumu mbalimbali ili kujenga familia na jamii bora zaidi.

“Maadhimisho haya yawe sehemu ya mabadiliko makubwa katika jamii yetu na kuondoa dhana potofu ya mfumo dume unaokandamiza makundi mengine wakiwemo wanawake na watoto. Sisi wababa ni walinzi na wafariji wakuu wa wanawake hivyo ni vyema tuwatunze, tuwapende na tuwaendeleze wake wake zetu”,amesema Katambi.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Dkt. Philemon Sengati amewataka wanaume kuwa mstari wa mbele kutetea haki za wanawake na watoto kwa kuepuka ukatili wa kijinsia n unyanyasaji wa wanawake na watoto ambao hupelekea majeraha makubwa ikiwa ni pamoja na ulemavu wa kudumu na kupoteza uhai.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA), Leticia Mourice Kapela amesema NACOPHA inasherehekea siku ya baba duniani kwa kuelekeza nguvu na mtazamo wa baba katika kuijenga na kuilinda familia ambayo ndani yake yumo mama au mtoto anayeishi na maambukizi ya VVU.

“Tunasherehekea kwa kumuangalia baba ambaye anaishi na mama au watoto ambao wanaendelea kupata huduma za UKIMWI zinazotolewa na serikali. Thamani na utashi wa baba katika kumlinda mama na mtoto anayeishi na maambukizi ya VVU ni jambo la msingi sana ambalo sisi NACOPHA tunalipigania kwa nguvu zote na wakati wote”,amesema Leticia.

“Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya kikatili ikiwemo mauaji ya akina mama ambao wanatumia dawa za ARV. Hii inadhihirisha wazi   kwamba pamoja na juhudi za serikali na wadau kupinga na kuondosha unyanyapaa, ubaguzi na matendo ya ukatili, matukio haya bado yapo hasa kwa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU. Matukio haya yanachangia kuchelewesha juhudi za serikali kuzifikia 95-95-95”,amesema.

Ameeleza kuwa baadhi ya matukio ya ukatili yanaunganishwa na mila na desturi zisizofaa hivyo amehimiza viongozi wa jadi na dini kubeba jukumu la kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuachana na mila na desturi zinazowaumiza wanawake na watoto sambamba na kuhimiza wanaume kupima afya zao,kulinda akina mama na watoto wanaotumia  huduma za UKIMWI.

Aidha ameshauri akina mama na watoto kutoa taarifa kwa vyombo husika pale matukio  ya ukatili yanapotaka kujitokeza au yanapotokea na serikali iendelee kuwashirikisha na kuwawezesha watu wanaoishi na maambukizi ya VVU katika kuandaa mikakati ya kupambana na ukatili wa kijinsia, kuendelea kufanya mapitio na maboresho ya sera,miongozo na sheria mbalimbali ili ziwe chachu na kuelekeza wadau kukabiliana na unyanyapaa na ukatili wa kijinsia.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akizungumza huku amebeba mtoto mgongoni ikiwa ni ishara ya kuunga mkono shughuli zinazofanywa na wanawake katika familia  kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akizungumza huku amebeba mtoto mgongoni ikiwa ni ishara ya kuunga mkono shughuli zinazofanywa na wanawake katika familia  kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA), Leticia Mourice Kapela akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021.
Meza kuu wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akiteta jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA), Leticia Mourice Kapela (kulia) , Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021.
Awali Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akiwasalimia wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya siku ya baba duniani. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Wanaume washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wakiandamana kutoka Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga kuelekea kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Wanaume washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe na vyombo wakiandamana kutoka Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga kuelekea kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga wakiwa kuni na ndoo za maji wakiandamana kutoka Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga kuelekea kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Waendesha bodaboda wakiwasili kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga wakati wa maandamano.
Washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga wakiwa wakionesha mabango yenye ujumbe mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Wababa wakipita mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini wakiwa wamebeba kuni, ndoo za maji na watoto katika uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Vijana wa skauti wakionesha mabango yenye ujumbe mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Mcheza ngoma ya Kisukuma maarufu Bugoyangi, bwana Mahona  kutoka kijiji cha Bugimbagu Shinyanga akicheza na nyoka anayejulikana kwa jina la Nderema kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga
Mcheza ngoma ya Kisukuma maarufu Bugoyangi, bwana Mahona  kutoka kijiji cha Bugimbagu Shinyanga akimuweka kwenye suruali yake nyoka anayejulikana kwa jina la Nderema kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga
Wananchi wakimshuhudia Mcheza ngoma ya Kisukuma maarufu Bugoyangi, bwana Mahona  kutoka kijiji cha Bugimbagu Shinyanga akicheza na nyoka kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga
Mchezo wa Igizo kutoka Kikundi cha Sanaa ya Maigizo VIWAWASHI kinachopatikana Mkoani Shinyanga ukiendelea kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga
Akina baba wakiwa wamebeba watoto mgongoni kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali kupitia NACOPHA kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali kupitia RAFIKI SDO kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akiwa ndani ya banda la upimaji afya kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akiwa katika banda la kuchangia damu salama kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Baba duniani ambayo nchini Tanzania yamefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Juni 20,2021 kwenye uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde -Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com