Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DIAMOND PLATNUMZ ACHAGULIWA KUWANIA TUZO ZA BET


Taasisi ya Hakimiliki Tanzania inapenda kumpongeza Msanii Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platinumz kwa kuchaguliwa kuwania tuzo  ‘Black Entertainment Television’ (BET) kwa mwaka 2021, katika kipengele cha ‘Best International Act’ Msanii aliyefanya vizuri  Kimataifa.

Kuchaguliwa kwa Diamond Platinumz kuwania tuzo hiyo ni heshima kwa taifa na Sanaa ya Muziki wa Bongo Fleva nchini, kwani hii inasaidia kutangaza nchi na  kuleta chachu katika ukuaji wa Muziki wa Bongo Fleva pamoja na kutoa hamasa kwa wasanii wa Tanzania kuongeza juhudi katika Sanaa ya Muziki .

COSOTA inatoa wito kwa Watanzania wote wa ndani na nje ya nchi kuwa Wazalendo na kumuunga mkono msanii huyo kwa kumtakia ushindi  wa kutwaa tuzo hiyo.

Pamoja na hayo mchakato wa kupatikana kwa mshindi katika kipengele cha ‘Best International Act’ hufanyika na wajumbe maalum ‘BET Voting Academy’ ambao huchaguliwa   na BET kutoka katika Sekta ya Sanaa na Burudani na hawa ndiyo hupiga  kura ya kumpata mshindi kwa kuangalia mafanikio  na ushawishi wa msanii huyo kwa mwaka huo ndani na nje ya nchi . Kundi hili ndiyo hutoa maamuzi ya kumpata mshindi.

Hata hivyo  unaweza kumpigia kura  Diamond kupitia mtandao wa BET  na  kusambaza hashtags yenye jina lake (#DiamondPlatinumz) katika mitandao ya kijamii, ili kumwongezea nafasi ya ushindi.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Juni 27, 2021 katika Mjini wa Los Angeles nchini Marekani.


Imetolewa na:
Anitha Jonas
 
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Elimu na Uhusiano




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com