Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa Juni 11,2021 amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa na kuteua wengine. Katika mabadiliko hayo , amemteua Bi. Batilda Salha Buriani kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuchukua nafasi ya Ally Hapi ambaye anahamia mkoa wa Mara huku aliyekuwa Katibu Tawala wilaya ya Simanjiro, Zuwena Omari Jiri akiteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Mara , Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi anahamia Mkoa wa Mwanza ambapo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila uteuzi wake umetenguliwa.
Social Plugin