NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI imesema haitawavumilia watumishi wa afya na watendaji wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakiwanyanyasa wazee wanapokwenda kupata huduma kwenye maeneo yao ya kazi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora dokta Batilda Buriani alipokutana na viongozi wa dini na wazee wa mkoa huo kwa nia ya kujitambulisha tangu ateuliwa kushika wadhifa huo na pia kupokea changamoto zinazowakabili ili aweze kuzitafutia ufumbuzi.
Alisema Serikali ya Mkoa chini ya uongozi wake haitawafumbia macho watumishi wanatoa lugha na kauli zisizostahili kwa wazee na watu wengine waofika kwenye maeneo yao ya kazi kupata huduma.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema huduma za Afya ni muhimu sana kwa wazee kwani walio wengi wamekuwa wanakabiliwa na magonjwa ya mara kwa mara hivyo wanahitaji uangalizi na matunzo maalumu na ya kitaalamu.
Alisema Serikali ya Mkoa itahakikisha Wazee wanapewa kipaumbele katika kupata huduma za kiafya kwa haraka na zilizo bora ikiwa ni pamoja na kuhakikisha madirisha ya Wazee yanakiweko katika hospitali, zahanati na vituo vyote vya Afya
Halikadhalika alielekeza zikiwemo Hospitali, Benki na Tanesco na Idara nyingne kuwapa kipaumbele Wazee na Viongozi wa Dini wanapofika kupata huduma.
Mkuu wa Mkoa aliwaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha kunakuwa na madirisha ya Wazee katika Hospitali Zahanati na Vituo vya Afya ilii Wazee wasikae foleni wanapoenda kupata huduma,
Katika risala ya wazee hao iliyosomwa na Willfred Mrutu walisema kuwa walilalamikia kutopata dawa kwenye vituo vya kutolea huduma pamoja na baadhi ya watumishi kuwatolea lugha mbaya,