Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Innocent Bashungwa akizungumza wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari |
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Innocent Bashungwa ameagiza Chama cha Maafisa Habari, Uhusiano na
Mawasiliano Serikalini kusimamia utekelezaji wa Maazimio ya Kikao kazi
kilichofanyika hivi karibuni Jijini Mbeya.
Mhe.Bashungwa
ametoa agizo hilo Juni 17, 2021 Jijini Dodoma alipukutana na kufanya
mazungumzo na Viongozi wa Chama hicho ambao wamechaguliwa na Mkutano
Mkuu wa Mwezi Mei 2021 Jijini Mbeya kuongoza kwa muda wa miaka mitatu.
"Nawapongeza
kwa kuchaguliwa, nasisitiza mkatekeleze na kusimamia majukumu yenu
vyema, Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji mkuu wa
Serikali pamoja na wasaidizi wake watakaa pamoja na nyinyi mjadili
maazimio ya mkutano ule kwa kina, mkakati wa namna ya kutekeleza pamoja
na kuweka msisitizo unaohitajika"amesema Mhe.Bashungwa.
Kwa
upande wake Pascal Shelutete amesema kuwa TAGCO ni moja ya kiungo
muhimu katika kutoa habari za Serikali kwa jamii kupitia Maafisa Habari
pamoja na kuisimamia vyema Kada hiyo muhimu kwa nchi.
Social Plugin