TATIZO LA UMEME NJOMBE KUMALIZWA BAADA YA SIKU 28


Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Dkt. Medard Kalemani amesema changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara mkoani Njombe itakwisha baada ya siku 28.

Dkt. Kalemani ameyasema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Njombe (CCM),  Deo Mwanyika.

Mwanyika amehoji ni lini tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara mkoani Njombe litatatuliwa.

Akijibu swali hilo, Dkt. Kalemani amekiri suala hilo na kubainisha kuwa unakatika kwa sababu kuna matengenezo yanaendelea ambayo yatachukua siku 28.

Amesema katika maeneo ya Njombe na Ludewa kuna laini ya umeme ambayo inaongezwa na kwamba ujenzi huo umetengewa Sh270 milioni.

Amebainisha kuwa pia wametenga Sh Milioni 100 katika Mkoa huo kwa ajili ya ukarabati wa mitambo na kuimarisha umeme Makambako, Njombe na Ludewa.

“Niwahakikishie ndani ya muda nilioutaja hali ya umeme itaimarika kwa kiasi kikubwa,” Kalemani


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post