Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UMITASHUMTA YATOA SITA KWENDA SLOVENIA MASHINDANO YA DUNIA

Wanariadha kutoka mikoa mbalimbali wakiwa kwenye mashindano ya mbio za mita 1500 katika viwanja vya Chuo cha Walimu leo Juni 14, 2021 mjini Mtwara.

1  Mratibu wa mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA Leonard Thadeo akitoa maelekezo kwa waamuzi na waratibu wa michezo wa mikoa mbalimbali iliyoshiriki mashindano hayo leo Juni 14,2021 mjini Mtwara

1.  Makatibu wakuu wa Wizara (Habari, TAMISEMI, na Elimu) zilizoratibu mashindano ya UMISHUMTA na UMISSETA na Wakurugenzi wakikagua miundombiunu ya mashindano hayo kabla ya kuanza rasmi Juni 7,2021 mjini Mtwara



Na John Mapepele, Mtwara

Serikali imesema wanafunzi sita watakaofanya vizuri mashindano ya UMITASHUMTA upande wa Riadha yanayoendelea kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu mjini Mtwara watapelekwa katika mashindano ya kimataifa ya Shirikisho la Michezo ya Wanafunzi Duniani (ISSF) yatakayoanza Septemba mwaka huu nchini Slovenia

Hayo yasemwa na Mratibu wa UMITASHUMTA na UMISSETA Taifa, Leonard Thadeo wakati akiongea na waratibu wa michezo, makocha na walimu wa michezo kutoka mikoa yote inayoshiriki mashindano hayo ambapo amesisitiza kuzingatia kanuni zote za michezo huu ili kuwapata wachezaji wenye nidhamu na sifa watakaopeperusha vema bendera ya nchi yetu

“Hii ndiyo dhana ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa ya kutaka ufundishaji michezo kuanza kwenye shule za Awali,Msingi, Sekondari na Vyuo ili kupata washiriki wengi walionolewa vizuri kwenye mashindano ya kimataifa kama yanavyofanya mataifa  makubwa”. Amefafanua Thadeo

Mhe. Majaliwa alisema wakati akifungua mashindano haya kuwa kupitia michezo na sanaa, wanafunzi watafunguliwa vipaji vyao ambavyo vikiendelezwa vema vitawapatia manufaa mazuri ya kitaaluma na ajira.

Katibu Mkuu wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt,Hassan Abbasi  amesisitiza kuwa Serikali imejipanga kuanzisha na kuboresha  vyuo vya michezo nchini ili  kupika na kunoa vipaji  vya wanamichezo na hatimaye  kuviuza duniani

“Mikakati ya Serikali kwenye Sekta ya Michezo kwa sasa ni kuhahakisha taaluma ya michezo inaboreshwa na inatolewa kwa kiwango cha kimataifa ili wanamichezo wetu wawe kwenye viwango vya kimataifa, tukumbuke kuwa michezo ni sayansi. “Amefafanua Dk Abbasi

Michezo ya leo kwenye riadha imehusisha mita 100 kwa wavuala na wasichana, mita 100 kwa wenye ulemavu ambayo imefika fainali na kumalizika, mita 1500 kwa wavulana na wasichana relay mita 400x4 na mchezo wa kurusha tufe ambao umefikia fainali ambapo mkoa wa Kigoma kwa upande wa wavulana na Manyara kwa wanawake walishinda.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com