Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAKULIMA MOROGORO WANUFAIKA NA MRADI WA KUONGEZA UZALISHAJI WA MPUNGA

 

Picha ikionesha Mfereji mkuu unaoepeleka maji mashambani katika skimu ya Msolwa Ujamaa.
Bi Wadara Kitada Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Mlimba Mkoani Morogoro akizungumza katika skimu ya Njage wakati wa ziara ya kikazi katika miradi ya kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga.
Picha Ikionesha Ghala la kuifadhia mazao katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Njage katika Halmashauri ya Mlimba


Sehemu ya Miundombinu katika skimu ya Kilimo cha Umwagiliaji Msolwa ujamaa Kilosa mkoani Morogoro.


NA; MWANDISHI WETU – MOROGORO

Wakulima katika skimu za kilimo cha umwagiliajiMvumi, Msolwa Ujamaa na Njage zilizopo katika Wilaya ya Kilosa, Kilombero na Halmashauri ya Mlimba Mkoani Morogoro,zimenufaika na ukamilishwaji wa ujenzi wa skimu za kilimo cha umwagiliajizilizopochiniyamradiwakuongezauzalishajiwazao la mpungauliyofadhiliwanaBankyaDunia.

Wakiongea katika nyakati tofauti baadhi ya wakulima katika skimu hizo, walisema hali ya kilimo katika skimu hizo haikuwa rafiki kabla ya kuwepo kwa ujenzi wa miundombinu hiyo ambapo kwasasa, hali ya kilimo ni nzuri kwani kuna uhakika wakupata wastani wa mavuno ya gunia 20 mpaka 30 kwa heka kutokana na uhakika na matumizi sahihi ya maji katika misimu tofauti ya kilimo.

Bi Mwanaisha Kaluwa mkulima katika Skimu ya Mvumi Wilayani kilosa amesema “Naishukuru Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kwa kutuletea mradi wenye manufaa kwetu sisi wakulima lakini Ombi langu ni kwamba Serikali itutafutie masoko ya uhakika kwani kwa sasa tunauza kupitia madalali ambao wanatuumiza sana ,hawatumii vifungashio halali wanafunga kwa kutumia rumbesa, tunaomba sana Serikali isimamie mpunga uuzwe kwa kutumia mizani.” Alisema Bi. Mwanaisha.

Afisa kilimo wa Halmashauri ya Mlimba Bi WadaraKidata,akizungumzia skimu ya kilimo cha umwagiliaji Njage alisema kabla ya mradi skimu ilikuwana changamoto ya maji ambayo kwa sasa wanapata maji kwa wakati barabarani nzuri ambazo zinarahisisha mazao kufika ghalani na kwa wanunuzi kwa wakati na gharama nafuu.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mhandisi wa mkoa wa Umwagiliaji Morogoro Njanji Mlole,alisema kabla ya kukabidhi mradi huo ambao upo katika muda wam atazamio, mapungufu machache yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na kurekebisha mabanio na kuinua sehemu ya vipange vya barabara za skimu na kubadilisha ma karavati katika skimu ya Njage Mlimba,pamoja na kuingiza mfumo wa majisafi katika vyoo yatarekebishwa katika kipindi hicho kwa mujibu wa mkataba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com