WASABATO WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KUSAIDIA WALIOPATA AJALI BASI LA CLASSIC


Suzy Luhende, Shinyanga

Kanisa la Waadventista Wasabato mjini Shinyanga limetoa vifaa tiba katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kutibu watu waliopata ajali kwenye basi la Kampuni ya Classic lililokuwa likitokea nchini Uganda kwenda jijini Dare es salaam nchini Tanzania, ambalo baada ya kufika kijiji cha Buyubi kata ya Didia lilipata ajali na  kusababisha vifo vya kuwatu wanne huku wakijeruhiwa 20.
Wakitoa msaada wa vifaa hivyo viongozi wa kanisa hilo Ellyson Maeja ambaye ni Mzee wa kanisa na Amani Tibore Mwinjilisti wa kanisa hilo, walisema wameguswa na ajali hiyo iliyotokea leo majira ya saa 10 alfajiri, kwa sababu kulikuwa na wanafunzi waliokuwa wakisoma Chuo Kikuu cha Bugema Univesity nchini Uganda cha kanisa la Kisabato.

Akikabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh 300,000 (laki tatu) amesema kanisa limeona litoe msaada huo wa vifaa tibà na dawa ili viwasaidie majeruhi waliolazwa hospitalini hapo, ambapo amesema wengine wanaendelea vizuri wameruhusiwa, hivyo wamewapatia malazi hotelini kwa ajili ya kupumzika na sasa wanafanya taratibu za kusafirisha marehemu watatu waliokuwa wanaelekea Zanzibar.

"Tumeguswa sana nahii ajali kwani kulikuwa na wanafunzi waliokuwa wakisoma chuo kikuu Bugema Univesity, hivyo tumetoa vifaa tiba hivi ili viweze kuwasaidia majeruhi hawa ambavyo ni monitol 12 Bottle, Surgical Gloves 100, Examination Glove 100,Canula 24g,Canula 20, Canula 16g, Cotton Woul 5,Bondage dose 10,hivyo vitawasaidia kutibiwa ili waweze kupona",alisema Maeja.

Kaimu Katibu wa afya (SRRH) mkoa wa Shinyanga Iveta Mtesigwa amesema wamewapokea marehemu wanne na majeruhi 20 kutokana na ajali hiyo wanawake watatu na mwanaume mmoja wote wamehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

"Tumewapokea marehemu wanne na tumewahifadhi na majeruhi 20 ambao wanaendelea na matibabu, ila kuna majeruhi wengine wanne ambao wameumia kichwani wamepewa rufaa ya kwenda Bugando kwa ajili ya kufanyiwa vipimo zaidi",amesema Mtesigwa.

Mtesigwa amesema analishukuru kanisa kwa kutoa vifaa hivyo kwani baadhi ya vifaa hivyo vilikuwa vimeisha hivyo kwa kupatikana vifaa hivyo vitasaidia skuwatibu watu waliopata ajali, hivyo wanakaribisha na taasisi zingine zitakazoguswa kutoa.

Dkt. Ellyson Maeja akikabidhi vifaa tiba kwa Kaimu Katibu wa afya (SRRH) hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Iveta Mtesigwa vilivyotolewa na kanisa la Sabato mjini Shinyanga kwa ajili ya kusaidia watu waliojeruhiwa kwenye ajali ya basi la Classic

Kaimu katibu wa afya (SRRH) Mkoa wa Shinyanga Iveta Mtesigwa akizungumza baada ya kukabidhiwa vifaa tiba kwa ajili ya kusaidia watu waliopata ajali vilivyotolewa na kanisa la Sabato mjini Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post