Watoto wa Kanisa la International Evangelical Assembles of God Tanzania (IEAGT) Mjini Shinyanga, wakiwa kwenye kilele cha wiki ya watoto kanisani hapo.
Na Marco Maduhu, Shinyanga
Watoto wa Kanisa la International Evangelical Assembles of God Tanzania (IEAGT) Mjini Shinyanga, wamelaani migogoro ya wazazi ndani ya familia, ambayo wameeleza imekuwa ikiwaathiri watoto wengi kisaikolojia, na hata kufanya vibaya kwenye masomo yao.
Wamebainisha hayo leo kwenye kilele cha wiki ya watoto kanisani hapo, wakati wa usomaji wa risala yao.
Akisoma risala kwa niaba ya watoto wenzake Naomi Daudi, amewataka wazazi kuacha tabia ya kugombana majumbani tena wengine mbele ya watoto, ili kutowaathiri kisaikolojia na kuharibu ndoto zao, sababu ya kufanya vibaya masomo.
"Migogoro ya wazazi ndani ya familia imekuwa ikituharibu sana watoto kisaikolojia, na hata kutusababishia kufanya vibaya kwenye masomo yetu ," amesema Naomi.
"Tunaomba pia wazazi wakiwa majumbani na watoto, wawafundishe neno la Mungu, na siyo kuwaacha wakichat mitandao ya kijamii, pamoja na kutazama runinga muda mwingi, ili wawe na maadili mema,"ameongeza.
Katika hatua nyingine watoto hao waliiomba jamii ya Mkoa wa Shinyanga, kuacha kubagua watoto wa kike hasa kwenye suala la kurithi mali na kumiliki ardhi, bali watoto wote wana haki sawa ikiwamo na kupewa elimu.
Naye Mtoto Miriam Kajiba, akitoa Mahubiri, amewataka wazazi kuwalea watoto katika maadili mema, pamoja na kufuatilia maendeleo yao ya shule na kuwatia moyo ili wafanye vizuri.
Aidha amesema kwa watoto wale ambao wanafeli mitihani yao na kushindwa kuendelea na elimu ya juu, wazazi wasiwavunje moyo pamoja na kuwatolea lugha mbaya, bali wawapeleke kwenye vyuo vya ufundi ili watimize ndoto zao.
Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa hilo David Mabushi, amewataka wazazi na walezi, kupenda kuwalea watoto wao katika misingi ya imani, pamoja na kuwahimiza kuhudhulia mafundisho ya vijana kanisani.
Pia amesisitiza suala la ugawaji urithi kwa watoto wa kike, liwe linazingatiwa ndani ya jamii na kuacha kuwabagua, ikiwa watoto wote wana haki sawa bila ya kujali jinsia zao.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mchungaji wa Kanisa la International Evangelical Assembles of God Tanzania (IEAGT) la Mjini Shinyanga David Mabushi, akizungumza kwenye kilele cha wiki ya watoto Kanisani hapo.
Mtoto Miriamu Kajiba, akitoa Mahubiri kwenye kilele cha wiki ya watoto Kanisani hapo.
Naomi Daudi akisoma Risala kwa Niaba ya watoto wote Kanisani hapo IEAGT, kwenye kilele cha wiki ya watoto.
Watoto wa Kanisa la IEAGT wakiwa kwenye kilele cha wiki ya watoto kanisani hapo.

Waumini wa Kanisa la IEAGT wakiwa kwenye kilele cha wiki ya watoto Kanisani hapo, wakiangalia Program za watoto.

Usomaji wa Mafungu ya Biblia ambayo wamekalili kichwani ukiendelea.
Watoto wakiimba nyimbo.
Watoto wakiimba nyimbo.
Watoto wakionyesha Maigizo yenye mafundisho ya Dini.
Igizo likiendelea.
Kamati ya maadalizi wiki ya watoto Kanisani hapo, wakieleza namna walivyofanikisha Program hiyo.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.
Social Plugin