WAZIRI JAFO: TAKWIMU ZA WAMI RUVU ZINAISAIDIA SERIKALI KUCHUKUA TAHADHARI ZA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI
Friday, June 04, 2021
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo, amesema takwimu zinazotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu ni Muhimu kwa Sababu zimekuwa zikiisaidia Serikali hususani Wizara yake kuchukua Tahadhari kuhusu suala zima la Mabadiliko ya Tabia nchi kwenye vyanzo vya maji ikiwemo Mito na Mabwawa.
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo Mjini Dodoma kwenye Wiki ya mazingira alipotembelea Banda la Maoensho la Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu.
Amesema Rasilimali maji ni Muhimu kwa maendeleo na Ustawi wa Binadamu, hivyo ameitaka Bodi hiyo ya Maji katika Bonde la Wami Ruvu kuwa mstari wa Mbele kuiongoza Serikali kupitia Takwimu zake ili iweze kuchukua hatua stahiki za kukabiliana na athari za Mazingira kwenye vyanzo vya Maji.
“ Ofisi yenu ni muhimu sana, lakini inatusaidia vile vile kutoa tahadhari watu wasivamie vyanzo vya maji Kwa Sababu wakivamia Mambo yote yanakuja kuharibika, kwa mfano leo hii tunajenga lile bwana la Nyerere kama watu watavamia vyanzo vya Maji lile bwana litakuwa halijai ” Alisisitiza Wazir Jafo.
Kilele cha Wiki ya Mazingira Duniani kinatarajia kufikia kilele chake June 5, ambapo Serikali inatarajia kuzindua Kampeni Kabambe ya Kuhamasisha Jamii Kutunza na Kulinda Mazingira.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin