Picha haihusiani na habari hapa chini
Askari polisi katika kituo kidogo cha polisi Mbughuni mkoani Arusha,PC Damas ameuawa kwa kukatwa na panga kichwani wakati akijaribu kumkamata mtuhumiwa wa wizi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jastine Masejo amesema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa tano usiku katika Kijiji cha Makiba wakati askari huyo alipoenda nyumbani kwa mhalifu kwa lengo la kumkamata.
Amesema askari huyo alifariki dunia muda mfupi baada ya kuvuja damu nyingi.
"Askari wetu katika kituo kidogo cha polisi Mbughuni alikatwa panga kichwani na kufariki dunia baada ya kwenda nyumbani kwa mhalifu majira ya saa tano usiku lengo la kumkamata, hivi sasa polisi wanaoendesha operesheni ya kumsaka ili afikishwe kwenye vyombo vya dola", amesema Kamanda Masajo.
Amesema wakati wa harakati za kumkamata ndipo alipotokea mhalifu mwingine nyumba ya jirani ambaye alimkata panga moja kichwani askari huyo na kupoteza naisha.
Social Plugin