Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CRDB KUCHUKUA ZAIDI YA WANACHUO 50 TIA KAMPASI YA SINGIDA

Meneja wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Kampasi ya Singida Dkt. James Mrema akizungumza kwenye kongamano hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Binilith Mahenge akihutubia kwenye kongamano hilo.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Rasilimali Watu kutoka CRDB , Godfrey Rutasingwa akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Baadhi ya Maafisa watendaji wa CRDB wakifuatilia matukio kwenye Kongamano hilo.
Mkurugenzi Rasilimali watu CRDB Siaophoro Kishimbo akizungumza mwenye kongamano la kitaaluma la Taasisi ya Uhasibu nchini(TIA) Kampasi ya Singida.
Kongamano la CRDB Carrier Fair Day Singida likiendelea.
***
 Na Edina Alex - Singida
Benki ya CRDB nchini imetangaza kuchukua wanafunzi wapatao hamsini kutoka Taasisi ya Uhasibu nchini Tanzania, Kampasi ya Singida kwa ajili ya kuwajengea uwezo kwenye nyanja ya mafunzo kwa vitendo kabla ya kuingia rasmi kwenye soko la ajira.

Kwa mujibu wa benki ya CRDB utaratibu huo hufanyika kila mwaka kwa kuchukuwa takribani wanavyuo 600 kutoka vyuo mbalimbali ikiwemo TIA, lengo ni kuwandaa kwa kuwafanya kuwa mahiri kwenye soko la ajira.

Akizungumza hivi karibuni kwenye kongamano la 'CRDB Carrier Fair Day' lililofanyika kwenye ukumbi wa TIA Kampasi ya Singida Mkurugenzi Rasilimali Watu kutoka CRDB Siaophoro Kishimbo alisema wanafanya hayo ilikuchagiza ubora na kuwawezesha wanafunzi kukidhi haja ya soko kulingana na dunia ya sasa.

Aidha Kishimbo alisema kwa sasa benki hiyo imeanza rasmi kupanua wigo wake kwa kutoa mafunzo hayo kwa vitendo ili kuwajengea na kuboresha weledi wao kwa vitendo katika muktadha wa kuwaanda vema kuwa waajiriwa watarajiwa, wafanyabiashara, na wateja wa benki hiyo sasa na mbeleni.

"Kupitia kongamano hili tunawafundisha namna ya kupata Fedha ,kutunza Fedha ,kuzizoea Fedha ,na kuwafanyia Kasi ya mahojianoya papo kwa papo ili kupima ujuzi wao na kuandaa utayari Kabla hawajawa waajiriwa, "alisema Kishimbo.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Rasilimali Watu kutoka benki hiyo, Godfrey Rutasingwa alisema CRDB inaridhishwa na ushirikishwaji unaofanywa na sekta ya elimu kwa waajiri nchini kabla ya kuandaa mitaala.

"Maboresho makubwa na uwezo wa wanavyuo wengi wanapoajiriwa kwa Sasa ni matokeo ya Serikali kupitia sekta ya elimu kushirikisha ipasavyo waajiri kwenye kuandaa mitaala ambao ndio wapo kwenye soko la ajira,"alisema Rutasingwa.

Awali akifungua kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge aliombaa benki ya CRDB mbali ya kuwasaidia waajiriwa watarajiwa namna ya kulipokea soko la ajira vijana hao wasiache kupewa mafunzo ya namna ya kujenga uchumi wa Tanzania.

Alisema dhana ya waajiri na waajiriwa vinapaswa kuchagizwa na Tanzania kwenye kuwezesha vijana wake kuwa na elimu ya kutosha na weledi katika kujenga uchumi imara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com