Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla amewahakikishia Watanzania wote kwamba chanjo ni Salama.
DC Makalla aliyasema hayo leo Julai 29,20212 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi juu ya Covid-19 na Lishe kwa Jamii,
Alisema yeye binafsi anajisikia Vizuri baada ya kupata chanjo hiyo na akawashauri watanzania walio Dar es Salaam na wasio Dar es Salaam waende kupata chanjo hiyo ya hiari.
Alimwomba Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima kutorudi nyuma katika kutoa elimu na mapambano hayo ya Covid-19.
Aidha alitoa pongezi kwa niaba ya mkoa wa Dar es Salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kupokea chanjo hii ya Covid-19.
Kwa niaba ya wakuu wa Wilaya waliopo Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Fatma Almas Nyangasa alitoa Shukrani kwa Kuandaa kikao hicho pia alitoa Shukrani kwa Waziri wa Afya.
Mapema waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima alisema anaupongeza sana Mkoa wa Dar es Salaam kwa hatua mbalimbali wanazozichukua jinsi ya kukabiliana na Janga hili
Lakini Waziri Dorothy Gwajima alisema Chanjo hizi zisichukue siku kumi ziwe zimefika kwa wananchi na alisema sehemu itakoyolegalega utoaji wa chanjo hiyo watazichukua
Alisema Mkoa wa Dar es Salaam upo jirani kbs na Bohari Kuu ya Dawa (MSD)Kwa hiyo waende kuzichukua ila (MSD) itapeleka Chanjo hiyo kwa mikoa yote ya Tanzania.
Social Plugin