Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amesema hadi sasa jumla ya watu 29 wamefariki dunia kutokana na wimbi la tatu la Covid-19 huku jana Julai 22,2021 pekee kulikuwa na jumla ya wagonjwa wapya 176.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 23,2021 Dkt. Dorothy amesema takwimu hizo ni alizopata jana hivyo upo uwezekano vifo zaidi vikawa vimetokea.
“Itoshe kuwaambia kuwa ugonjwa upo na watu wanakufa, tusingependa kupeana hizi taarifa za vifo tuchukue tahadhari, kila mmoja wetu ajiulize unapofanya mambo kinyume na kuchukua tahadhari unalenga kumtesa nani,” amesema Dkt. Gwajima.
Idadi hiyo inafikisha Tanzania kuwa na jumla ya wagonjwa 858 wa Covid-19.
Social Plugin