Tanzania imeanza kutoa takwimu ya watu walioambukizwa virusi vya corona ambapo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amesema hadi kufikia Julai 8, 2021 jumla watu 408 walibainika kuwa na ugonjwa wa Corona huku 284 wakitumia mitungi ya Hewa ya Oksijeni.
Dk Gwajima ametoa taarifa hiyo leo Jumamosi Julai 10, 2021 wakati akitoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwenye mnada wa Msalato jijini Dodoma.
Rais Samia Suluhu Hassan mara kwa mara amekuwa akiwakumbusha Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na kujilinda dhidi ya wimbi la tatu la janga la corona.
Katika moja ya ziara yake akiwa njiani kutoka Dodoma Rais Samia alielezea kushangaa kuona mamia ya watu bila barakoa.
Social Plugin