Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

EVIH , NYOTA MPYA KUTOKA NIGERIA ANAYEKUJA KUUSHANGAZA ULIMWENGU WA MUZIKI AFRIKA MASHARIKI

Evans Oghenekaro Ambakederemo maarufu kwa jina la EVIH ni nyota mpya wa muziki kutoka nchini Nigeria ambaye anafanya vizuri kwa hivi sasa kutokea nchini humo.

Evih amewahi kufanya kazi kadhaa na moja ya kazi yake iliyofanya vizuri alishirikiana na msanii wa muziki kutoka Nigeria na mshindi wa tuzo ya BET katika kipengele cha Best international Act miaka kadhaa iliyopita,David Adeleke maarufu kwa jina la DAVIDO.

Licha ya kazi hiyo kufanya vizuri Evih ameamua kutanua wigo wa mashabiki zake kutoka Nigeria mpaka Afrika ya Mashariki kwa kuachia kazi yake aliyoipa jina la FOREIGN (SO WAVY) Ambayo inaambatana na safari yake nchini Tanzania na Kenya kwa ajili ya kuzuru katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni Afrika Mashariki akianzia nchini Tanzania.

Unaweza kufuatilia kazi zake kupitia chaneli yake ya youtube na pia kuwa karibu nae zaidi kwa kumfuata kupitia ukurasa wake wa Instagram na twitter kwa jina la @evihofficial.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com