Rais wa Chama cha Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA), John Bina amelipongeza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kuanzisha Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu Mwanza (Mwanza Precious Metals Refinery) kwa kiwango cha kimataifa cha asilimia 99.99%.
Rais huyo wa FEMATA ameyasema hayo leo Jumanne Julai 27, wakati akitembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Bina ametumia nafasi hiyo kuishauri STAMICO kuendelea kuelimisha Wananchi juu ya umuhimu wa Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu kwa wachimbaji wadogo kwani wachimbaji wengi wadogo hawana uelewa.
Aidha Bina amelipongeza Shirika la Madini la Taifa kwa kuendelea kuwa mlezi mzuri kwa wachimbaji wadogo.
Afisa Masoko wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mark Mahungo (kulia) akimwelezea Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina kuhusu Mkaa Mbadala 'Rafiki Briquettes' alipotembelea banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina akizungumza katika banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina akiangalia mwamba wenye madini alipotembelea banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin