Fredy Shoo maarufu Fresho enzi za uhai wake
Mkurugenzi wa Kampuni ya Fresho Investment Company (1999) Ltd ya Mjini Shinyanga Fredy Shoo maarufu Fresho amefariki dunia leo jioni Jumatano Julai 28,2021 wakati akiendelea kupata matibabu jijini Dar es salaam.
Mwekezaji Mzawa Fredy Shoo ndiye mmiliki wa kiwanda cha kuchambulia pamba , kiwanda cha vifungashio na kiwanda cha kuchakata mafuta ya pamba pamoja na uwanja Mpya wa Kisasa uliopewa jina la ‘Fresho Complex’ uliopo katika eneo la Ugweto kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Mungu Ailaze Mahali Pema Peponi Roho ya Marehemu Fresho. Amina
Social Plugin