Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi (kulia) akimwelezea Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya kuhusu Akaunti ya Hodari ambayo ni akaunti maalumu kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na wa kati wakiwemo Machinga, Bodaboda, Mama lishe, Wafanyabiashara kwenye masoko, Mafundi vyerehani, Seremala, Wachimbaji Wadogo wa Madini na makundi mengine. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi (kulia) akimwelezea Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (wa pili kushoto) kuhusu Akaunti ya Hodari ambayo ni akaunti maalumu kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na wa kati wakiwemo Machinga, Bodaboda, Mama lishe, Wafanyabiashara kwenye masoko, Mafundi vyerehani, Seremala, Wachimbaji Wadogo wa Madini na makundi mengine.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi (kulia) akimwelezea Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (wa pili kushoto) kuhusu huduma zinazotolewa na Benki ya CRDB alipotembelea banda la CRDB Bank kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya CRDB imeshiriki Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga ambapo imetumia fursa hiyo kuwaomba Wananchi kuchangamkia fursa ya Akaunti ya Hodari ambayo ni akaunti maalumu kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na wa kati wakiwemo Machinga, Bodaboda, Mama lishe, Wafanyabiashara kwenye masoko, Mafundi vyerehani, Seremala, Wachimbaji Wadogo wa Madini na makundi mengine.
Akielezea kuhusu Akaunti ya Hodari kwa Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akitembelea banda la CRDB Bank, Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi amezitaja sifa za Akaunti ya Hodari kuwa ni pamoja na kutokuwa na ada ya mwezi kuendesha akaunti.
"Sifa kuu za Akaunti ya Hodari ni kwamba kiasi cha kufungulia akaunti ni shilingi 5,000/=, haina gharama za kuendesha akaunti, haina ada ya mwezi,haina ada ya kutolea pesa tawini,haina makato ya miamala ya Simbanking, haina makato ya Internet Banking, haina malipo yanayopokelewa kupitia LIPA HAPA na haina makato ya kutoa pesa ATM",ameeleza Mwanahamisi.
Mwanahamisi ameeleza kuwa Benki ya CRDB inawawezesha Mikopo Wachimbaji Wadogo wa Madini na Wajasiriamali kwani furaha ya Benki ya CRDB ni kuona Wachimbaji Wadogo wa Madini na Wajasiriamali wanakua kiuchumi.
Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yamefunguliwa na Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Jumapili Julai 25,2021.
Prof. Manya ameipongeza na kuishukuru Benki ya CRDB kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika shughuli mbalimbali na kwa upande wa Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga wamekuwa miongoni mwa wadhamini wa maonesho hayo.
Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayoongozwa na kauli mbiu “Uwekezaji wa Madini na Viwanda Shinyanga kwa Uchumi Endelevu” yameanza tarehe 23 Julai, yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 1 Agosti, 2021 katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.