Msanii wa muziki mwenye asili ya nchini Kenya ambaye amekuwa akifanya Muziki kwa miaka kadhaa na kuelekeza talanta yake nchini Tanzania kwa kufanya kazi na watayarishaji wa muziki mahiri hapa nchini Tanzania hasa katika tasnia ya muziki wa Hip Hop kama vile Deey Classic pamoja na Q The Don.
Jamaa Flani a.k.a Jflani ni moja ya msanii mwenye mtazamo chanya sana katika muziki
wake jambo ambalo linamfanya kuwa moja kati ya watu wanaopenda ubora zaidi
katika kazi zake na kwa mara ya kwanza Jflani anakuletea kazi yake mpya ambayo
anakiri kuifanya katika kiwango cha juu zaidi kuwahi kufanya wimbo unaitwa
Nitakuwezaje akiwa amemshirikisha mrembo Icome na video kutayarishwa na
kuongozwa na Director Simon SPK chini ya Nyasha Music.
Karibu kutazama wimbo huu mpya na kushare pamoja na marafiki na unaweza kuwa karibu zaidi na instagram ya @jflani ili kufahamu zaidi na zawadi zitatolewa kwa atakayekuwa makini zaidi.
Social Plugin